Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALAMA

Mali: Elysee yatangaza kifo cha mwanajeshi wa Ufaransa aliyeuawa katika mapigano

Mwanajeshi wa Ufaransa aliuawa katika mapigano nchini Mali Ijumaa asubuhi, ofisi ya rais wa Ufaransa ilitangaza tangaza Ijuma usiku, ikielezea "huzuni" kutoka kwa wais Emmanuel Macron, ambaye "amesema Ufaransa itaendelea hadi mwisho katika vita vyake dhidi ya ugaidi".

Kifo cha Maxime Blasco kinafikisha idadi ya wanajeshi 52 wa Ufaransa waliouawa huko Sahel tangu mwaka 2013 katika operesheni za kupambana na jihadi, Serval na kisha Barkhane.
Kifo cha Maxime Blasco kinafikisha idadi ya wanajeshi 52 wa Ufaransa waliouawa huko Sahel tangu mwaka 2013 katika operesheni za kupambana na jihadi, Serval na kisha Barkhane. AFP - DAPHNE BENOIT
Matangazo ya kibiashara

Maxime Blasco, wa Kikosi cha 7 cha Alpine Chasseurs de Varces (Isère), aliuawa katika mapigano "dhidi ya kundi la kigaidi lenye silaha". Kulingana na makao makuu ya jeshi la Ufaransa, mwanajeshi huyo aliuawa "wakati wa operesheni ya upelelezi iliofanywa na kikosi cha Barkhane huko Gourma, nchini Mali", katika mkoa wa Gossi, karibu na mpaka kati ya Mali na Burkina Faso.

"Wapiganaji wa kundi la kigaidi waligunduliwa na dege isiyo na rubani aina ya Reaper mapema asubuhi, katika msitu wa N'Daki. Doria ya helikopta mbili za kushambulia iliingilia kati haraka ili kuwaangamiza magaidi hao, " makao makuu ay jeshi la Ufaransa imeongeza.

Kifo chake kinafikisha idadi ya wanajeshi 52 wa Ufaransa waliouawa huko Sahel tangu mwaka 2013 katika operesheni za kupambana na jihadi, Serval na kisha Barkhane. Januari 2, askari wawili akiwemo mwanamke, wote kutoka kikosi cha 2 hussards de Haguenau (Bas-Rhin), waliuawa katika gari lao la kivita (LAV) baada ya kilipuzi kulipuka" wakati operesheni za upelelezi na ujasusi.

Siku tano kabla, wanajeshi watatu wa kikosi cha 1 cha wawindaji wa Thierville-sur-Meuse (Meuse) pia waliuawa kwa bomu lililotengenezwa kienyeji. Mashambulizi yote mabaya yalidaiwa na Kundi la GSIM, lenye mafungamano na Al-Qaeda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.