Pata taarifa kuu
GAMBIA-HAKI

Gambia: Familia za wahanga zadai haki

Tume inayohusika na kutoa mwanga juu ya uhalifu uliofanywa chini ya utawala wa rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh iliahirisha jana, Alhamisi, Septemba 30, kutangazwa kwa ripoti yake ya mwisho, kwa sababu ya ukosefu wa muda. Kwa upande wa waathiriwa na familia zao wamesema kuahirishwa huko sio ishara nzuri.

Gambia: maandamano huko Banjul Desemba 2017 kwa kutoa heshima zao kwa Deyda Hydara, mwandishi wa habari aliyeuawa katika utawala dikteta Yahya Jammeh.
Gambia: maandamano huko Banjul Desemba 2017 kwa kutoa heshima zao kwa Deyda Hydara, mwandishi wa habari aliyeuawa katika utawala dikteta Yahya Jammeh. RFI / Claire Bargelès
Matangazo ya kibiashara

Raia nchini Gambia wanaendelea kusubiri ukweli kwa uhalifu uliyotokea katika utawala wa rais wa zamani wa nchi hiyo Yahya Jammeh. Tume ya Ukweli na Maridhiano, ambayo ilianza kazi mwezi Oktoba 2018, imeelezea kuahirishwa kitangazwa kwa ripoti kumetokana na wingi wa nyaraka zinatakiwa kukusanywa: Ni ripoti ambayo imekusaya vitabu 16, kwa sababu tangu Januari 2019, tume imesikia mashahidi karibu 400 na kukusanya taarifa karibu 3,000.

Lakini hii ni mara ya tatu kutangazwa kwa ripoti hii inayosubiriwa kunaahirishwa, na inakuja katika hali ya kisiasa tete kwani mwanzoni mwa mwezi Septemba chama cha rais Adama Barrow kilitia saini kwenye mkatanba wa ushirikiano na kile cha rais wa zamani Yahya Jammeh.

Kwa familia za wahanga kama Baba Hydara, uahirishaji huu mpya haueleweki. Alimpoteza baba yake, mwanahabari maarufu Deyda Hydara, katika mauaji mnamo mwaka 2004. "Tangu mwezi Julai imesemwa kwamba ripoti hiyo imewasilishwa kwa rais na hadi sasa hakuna chochote.

Kwa sisi wahanga, ni shida kidogo na wakati huo huo tuna wasiwasi, kwa sababu hatujui sababu halisi. Uhalifu mwingi uliofanywa, Yahya Jammeh ndiye alikuwa mdhamini. Miongoni mwa uhalifu huu, mauaji ya baba yangu. Na hatukupata haki. Uhusiano huu huashiria vitu vingi.

Pamoja na mapendekezo haya, serikali italazimika kuamua hatima ya wahalifu kadhaa ambao wamefanya uhalifu wa kutisha. Ushirikiano huu ni kitu, pia, ambacho kinaweza kuifanya serikali kujifikiriakabla ya kuchukuwa maambuzi ... haifai kabisa, kwa sababu wafuasi wengi wa chama cha rais wa zamani, dikteta Yahya Jammeh ni wafuasi wa chama

chake rais wa sasa, ambacho sasa kimeshirikiana na chama cha rais wa zamani, kwa hivyo itakuwa ngumu kuhukumu baadhi yao ”.

Ushirikiano kati ya chama tawala cha rais Adama Barrow na kile cha dikteta wa zamani Yahya Jammeh unakuja miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa urais mnamo mwezi Desemba na inatia shaka juu ya nia ya kumshtaki kiongozi huyo wa zamani kwa madai ya ukiukaji wa haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.