Pata taarifa kuu

Mali: Mwanajeshi wa Ufaransa auawa katika shambulio la bomu Gao

Mwanajeshi wa Ufaransa aliuawa siku ya Jumamosi nchini Mali katika shambulio la bomu kwenye kambi ya kijeshi ya Operesheni Barkhane huko Gao, Ikulu ya Elysee imetangaza Jumapili hii Januari 23.

Mwanajeshi wa Ufaransa aliuawa Jumamosi Januari 22 huko Gao, Mali, katika shambulio la bomu kwenye kambi ya jeshi ya Operesheni Barkhane.
Mwanajeshi wa Ufaransa aliuawa Jumamosi Januari 22 huko Gao, Mali, katika shambulio la bomu kwenye kambi ya jeshi ya Operesheni Barkhane. AP
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kwa vyombo vya habari inaeleza kwamba Rais Emmanuel Macron amehuzunishwa na kifo cha Brigedia Alexandre Martin, wa kikosi cha 54 cha jeshi la Hyères, na "inathibitisha dhamira ya Ufaransa ya kuendelea na mapambano dhidi ya ugaidi katika eneo hilo, pamoja na washirika wake".

Rais wa Ufaransa Emanuel Macron amewapongeza askari waliokuwa zamu katika eneo hilo, kwa ujasiri walioonesha na kuthibitisha azma ya Ufaransa kuendeleza mapambano dhidi ya ugaidi katika eneo hilo.

Mwanajeshi huyo aliyefariki Jumamosi alasiri ametimiza idafi ya wanajeshi 53 wa Ufaransa waliouawa katika mapigano katika eneo la Sahel tangu 2013. Wanajeshi wengine tisa wa Ufaransa "walijeruhiwa kidogo" katika shambulio hilo", makao makuu ya jeshi la Ufaransa imesema katika taarifa.

Kambi hiyo ililengwa muda mfupi kabla ya saa 5:00 usiku kwa saa za Paris na "mabomu kadhaa " kutoka kwa eneo lililoko umbali wa "kilomita tano hadi sita kuelekea kaskazini mashariki", msemaji wa makao makuu ya jeshi la Ufaransa, Kanali Pascal Ianni, ameliambia shirika la habari la AFP.

Jeshi la Ufaransa "mara moja lilifanya msako na kushambulia kwa helikopta kwa lengo la kuwaangamiza washambuliaji", ameongeza Kanali Ianni. Hta hivyo wameangamizwa, amesema, bila maelezo zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.