Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Ufaransa yajiandaa kutoa wanajeshi wake Timbuktu

Wanajeshi wa Ufaransa wanajiandaa kuondoka katika mji wa kihistoria wa Timbuktu nchini Mali, baada ya Paris kutuma wanajeshi wake kukabiliana na makundi ya kijihadi katika eneo la Sahel, miaka minane iliyopita.

Kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa, Barkhane.
Kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa, Barkhane. AP - Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Ufaransa zaidi ya 5,000 vilitumwa mara ya kwanza katika êneo LA Sahel pamoja na Mali  na rais wa zamani Francois Hollande Februari mwaka 2013 kukabiliana na wanajihadi waliokuwa wamedhibiti mji huo.

Baada ya kuwasili kwa wanajeshi wa Ufaransa, kwa ushirikiano na wale wa Mali, walifanikiwa kuukomboa mji hui ambao kwa miezi minane, ulikuwa chini ya wapiganaji wa Kiislamu.

Kuondoka kwa vikosi vya Ufaransa katika kambi yake mjini Timbuktu kunazua maswali kuhusu usalama wa êneo hilo la Kaskazini mwa Mali, siku zijazo baada ya kuondoka kwa wanajeshi hao.

Mwezi Juni, rais Emmanuel Macron alutangaza mpango wa kupungiza vikosi vya Ufaransa nchini na katika êneo la Sahel kuanzia mapema mwaka ujao, huku vikosi vinavyotarajiwa kusalia, vinatarajiwa kuwa chini ya Elfu tatu.

Mbali na Timbuktu, vikosi vya Ufaransa vimeondoka katika kambi za Kidal na Tessalit, Kaskazini mwa Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.