Pata taarifa kuu

AFCON 2022: Watu wanane wauawa, 50 wajeruhiwa katika mkanyagano Yaounde

Watu wanane wamepoteza maisha na wengine 38 wamejeruhiwa, baada ya kutokea kwa mkaganyano nje ya uwanja wa michezo wa Olembe jijini Yaounde, Jumatatu usiku, kabla ya kuanza kwa mechi ya hatua ya 16 kat ya wenyeji na Comoro, kutafuta ubingwa wa soka kwa mataifa ya Afrika.

Mkanyagano umesababisha vifo vya watu wanane katika uwanja wa soka wa Olembe huko Yaoundé, kabla ya mechi kati ya Cameroon na Comoro.
Mkanyagano umesababisha vifo vya watu wanane katika uwanja wa soka wa Olembe huko Yaoundé, kabla ya mechi kati ya Cameroon na Comoro. © N. Bamba/RFI
Matangazo ya kibiashara

Serikali nchini Cameroon imethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, baada ya kuonekana kwa picha na mikanda ya vídeo kwenye lango la uwanja huo, zikionesha mashabiki wa soka wakikanyagana.

Rais Paul Biya ameagiza uchunguzi kufanyika kubaini mazingira yaliyosababisha tukio hilo, huku Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF, likisema linafuatilia kilichotokea kwa karibu.

Licha ya uwanja huo kuwa na uwezo wa kuwaingiza watu Elfu 60, kwa sababu ya janga la Covid-19, kamati andalizi ya mashindano haya; iliagiza kuwa asilimia 60 ya watu ndio watakaoruhusiwa kuingia uwanjani na wakati Cameroon inacheza, asilimia 80 ya mashabiki ndio watakaoruhusiwa  katika mechi hiyo.

Matukio kama haya yamekuwa yakishuhudiwa mara kwa mara, na kusababisha vifo na majeraha ya watu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.