Pata taarifa kuu
SOKA-MICHEZO

Misri yajiunga na timu nyingine tano ambazo zinaingia katika 16 bora ya AFCON

Bingwa mara saba wa taji la soka kwa mataifa ya Afrika Misri, imefuzu katika hatua ya 16 bora, kutafuta ubingwa wa mwaka huu, baada ya kuishinda jirani zao Sudan bao 1-0 katika mechi yake ya mwisho ya kundi D.  

Mohamed Salah na Mohamed Abdelmoneim (katikati) wakishangilia bao la mwisho dhidi ya Sudan kwenye mechi ya AFCON 2022.
Mohamed Salah na Mohamed Abdelmoneim (katikati) wakishangilia bao la mwisho dhidi ya Sudan kwenye mechi ya AFCON 2022. REUTERS - MOHAMED ABD EL GHANY
Matangazo ya kibiashara

Timu nyingine katika kundi hili Nigeria, imemaliza katika nafasi ya kwanza katika kundi hilo kwa alama 9 na kufuzu baada ya kuifunga Bissau 2-0.

Mataifa mengine yaliyofuzu katika hatua ya 16 ni pamoja na wenyeji Cameroon,  Burkina Faso, Gabon, Senegal, Cape Verde, Guinea, Morocco na Malawi.

Ratiba ya timu zitakazofuzu zinatarajiwa kufahamika Alhamisi usiku, baada ya mechi za mwisho.

Kundi E 

Cote Dvoire vs Algeria

Sierra Leon vs Equitorial Guinea

Kundi F

Gambia vs Tunisia

Mali vs Mauritania

Katika hatua nyingine, wachezaji 12 kati ya 28 wa Tunisia, wameambukizwa virusi vya Corona, kuelekea mechi yao ya mwisho ya kundi F dhidi ya Gambia siku ya Alhamisi usiku.

Hatua hiyo imeiacha Tunisia na wacheaji 16 kuelekea katika mechi hii, miongoni mwa wachezaji muhimu waliombukizwa ni Wahbi Khazri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.