Pata taarifa kuu

Fainali ya kwanza ya shirikisho barani Afrika kuchezwa wikendi hii

Klabu ya Renaissance Berkane ya nchini Morocco itakuwa mwenyeji wa Zamalek ya nchini Misri katika fainali ya kwanza kuwania ubingwa wa shirikisho barani Afrika siku ya Jumapili.

Klabu ya Renaissance Berkane itakuwa mwenyeji wa fainali ya shirikisho barani Afrika wikendi hii.
Klabu ya Renaissance Berkane itakuwa mwenyeji wa fainali ya shirikisho barani Afrika wikendi hii. CAF
Matangazo ya kibiashara

USM Alger ya nchini Algeria ambayo ilisusia mechi zote za semi fainali kulalamikia hatua ya ramani ya Morocco kuchapishwa kwenye mavazi ya wachezaji wa Berkane, imeitaka mahakama ya mizozo ya michezo (CAS) kutupilia mbali uamuzi huo wa kuchezwa kwa fainali hiyo.

Aidha, USM Alger pia inataka mechi ya mzunguko wa kwanza kuwania ubingwa huo ambayo imepangwa kuchezwa katika wa manispa wa kaskazini mashariki mwa Morocco kuhairishwa.

USM Alger walishinda Kombe la Shirikisho la 2023.
USM Alger walishinda Kombe la Shirikisho la 2023. © Courtesy of CAF

Katika hatua nyingine Zamalek ilitaka shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kuwabadilisha waamuzi wa video walioteuliwa kusimamia mechi ya mzunguko wa kwanza na wengine kutoka mataifa mengine.

Mzozo kuhusu mavazi ya kucheza ulianza siku mbili kabla ya mzunguko wa kwanza iliopangwa kupigwa tarehe 21 ya mwezi Aprili baada ya maofisa nchini Algeria kunasa mavazi yaliokuwa na ramani ya Sahara Magharibi.

Wachezaji wa klabu ya Zamalek
Wachezaji wa klabu ya Zamalek © Courtesy of CAF

Morocco kwa sehemu kubwa imekuwa ikitawala eneo la Sahara Magharibi tangu mwaka wa 1975 lakini nchi ya Algeria imekuwa ikipinga hatua hiyo ya Morocco ikitaka eneo hilo kutangazwa kuwa nchi huru.

CAF iliitaka mamlaka nchini Algeria kurejesha mavazi hao na ilipofanya hivyo, Berkane walikataa kucheza hali ambayo ilisababisha CAF kuwapa alama tatu.

Wachezaji wa klabu ya  Renaissance Berkane katika mechi ya awali.
Wachezaji wa klabu ya Renaissance Berkane katika mechi ya awali. © Courtesy of CAF

Algeria ilitetea hatua yake kwa misingi kwamba mavazi hao yalikuwa na ujumbe wa kisiasa hatua ambayo ni kinyume na sheria za CAF na FIFA.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.