Pata taarifa kuu

Soka: PSG yatangazwa bingwa wa ligi ya Ufaransa kwa mara ya kumi na mbili katika historia yake

Paris Saint-Germain iimetangazwa bingwa wa ligi ya Ufaransa kwa mara ya 12 katika historia yake baada ya kushindwa kwa mpinzani wake Monaco dhidi ya Lyon (2-3) siku ya Jumapili Aprili 28. Wakiwa na pointi kumi na mbili mbele ya Monegasques, Paris saint Germain wanaongozwa kwa kasi kubwa na hakuna timu inayoweza kuthubutu kuwapiku, zikiwa zimesalia siku tatu pekee za mechi ya Ligue 1. 

Wachezaji wa PSG wakisalimiana na mashabiki wao baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Le Havre (3-3) Uwanja wa Parc des Princes, Aprili 27, 2024.
Wachezaji wa PSG wakisalimiana na mashabiki wao baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Le Havre (3-3) Uwanja wa Parc des Princes, Aprili 27, 2024. © AFP / FRANCK FIFE
Matangazo ya kibiashara

Klabu hiyo ya mji mkuu sasa inaweza kuangalia malengo yake matatu kwa vile bado iko mbioni katika Ligi ya Mabingwa (nusu fainali dhidi ya Borussia Dortmund Mei 1 na Mei 7) na kombe la Ufaransa (fainali dhidi ya Lyon Mei 25).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.