Pata taarifa kuu

Soka: Mvutano waibuka kuhusiana na kocha mpya wa timu ya taifa ya Cameroon

Shirikisho la soka la Cameroon (Fécafoot) lilmeshutumu siku ya Jumatano uamuzi wa "upande mmoja" uliochukuliwa siku moja kabla na serikali kwa kumteua Mbelgiji Marc Brys kocha wa timu ya taifa ya wanaume kuchukua nafasi ya Rigobert Song.

Kocha mpya, Marc Brys, anarithi mikoba ya Rigobert Song ambaye mkataba wake ulimalizika mwishoni mwa mezi wa Februari na haukuongezwa tena na rais wa Simba wa Nyika, Samuel Eto'o.
Kocha mpya, Marc Brys, anarithi mikoba ya Rigobert Song ambaye mkataba wake ulimalizika mwishoni mwa mezi wa Februari na haukuongezwa tena na rais wa Simba wa Nyika, Samuel Eto'o. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Shirikisho la Soka la Cameroon limegundua, wakati huo huo na Wacameroon wote, juu ya kuteuliwa kwa nyadhifa za uwajibikaji ndani ya Uchaguzi wa Kitaifa wa Kandanda ya Wanaume" Fécafoot imesema, na kubainisha kuwa imepigwa na "mshangao mkubwa", katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa Facebook. .

Kulingana na Shirikisho hili, uteuzi huu unapinga agizo la rais "kuhusu kupanga na uendeshaji wa chaguzi za kitaifa za kandanda", ambalo linabainisha kuwa usimamizi wa michezo wa timu ya za taifa uko chini ya uwezo wa Fécafoot. Shirikisho hili linahakikisha "kwamba litafahamisha bila kuchelewa juu ya hatua ambayo inakusudia kuchukuwa". 

Kocha mpya, Marc Brys, 61, ambaye aliyeteuliwa siku ya Jumanne katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Waziri wa Michezo, anarithi mikoba ya Rigobert Song ambaye mkataba wake ulimalizika mwishoni mwa mwezi wa Februari na haukuongezwa tena na rais wa timu ya taifa ya soka ya Cameroon, Smba wa Nyika, Samuel Eto' o.

Huyu ni mwalimu wa tatu wa Ubelgiji kuchukua jukumu la kuinoa timu ya taifa ya soka ya Cameroon. Aliyetangulia alikuwa Hugo Broos, ambaye aliipeleka timu hii kutwaa taji la Kombe la Afrika mwaka wa 2017.

Cameroon iliondolewa katika hatua ya 16 bora ya AFCON mwezi Januari 2024, kwa kuchapwa na Nigeria 2-0. Kocha huyo mpya atakuwa na dhamira kuu ya kufanya Simba kufuzu kwa toleo lijalo la mwaka 2025 na Kombe la Dunia la mwaka 2026.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.