Pata taarifa kuu

Choguel Maïga: Ufaransa ilitaka kuigawanya Mali katika sehemu mbili

Waziri Mkuu wa Mali Choguel Kokalla Maïga aliishutumu Ufaransa siku ya Jumatatu kwa kufanya kazi ya kuigawanya nchi yake kupitia ahadi yake ya kijeshi, katika mashtaka mapya makali mbele ya wanadiplomasia walioko Bamako.

Waziri Mkuu wa Mpito wa Mali, Choguel Maïga, mjini New York, Septemba 26, 2021.
Waziri Mkuu wa Mpito wa Mali, Choguel Maïga, mjini New York, Septemba 26, 2021. © AFP - KENA BETANCUR
Matangazo ya kibiashara

Bw. Maïga, kiongozi wa serikali iliyowekwa na wanajeshi waliochukuwa madaraka kupitia mapinduzi mara mbili mfululizo mnamo Agosti 2020 na Juni 2021, aliishambulia Ufaransa kwa zaidi ya dakika 45, mbele ya wanadiplomasia waliokusanyika kwa ombi lake, bila kwenda mbali na kuomba kwa uwazi kuondolewa kwa kikosi cha kupambana na jihadi cha Barkhane kinachoongozwa na Paris.

"Baada ya wakati wa furaha" mnamo 2013 wakati wanajeshi wa Ufaransa walipokomboa eneo la kaskazini mwa Mali, ambalo lilikuwa chini ya udhibiti wa makundi ya wanajihadi, "uingiliaji kati baadaye uligeuka kuwa operesheni ya kugawanya Mali ambayo (ilijumuisha) sehemu ya eneo letu, ambapo magaidi walipata wakati wa kukimbilia, kujipanga upya ili kurejea kwa nguvu kuanzia 2014", alisema.

Katika muktadha wa mvutano mkali kati ya Paris na Bamako, alitoa mfano wa Vita vya Pili vya Dunia akisema: "Je, Wamarekani hawakuikomboa Ufaransa? (...) Wafaransa walipoamua kuwa (uwepo wa Marekani nchini Ufaransa) si lazima tena, wakawaambia Wamarekani waondoke, je wamarekani walianza kuwatukana Wafaransa? ", amejiuliza

Ufaransa yaunga mlkono vikwazo vya ECOWAS

Tangu Jumuiya ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ilipoiwekea vikwazo Mali mnamo Januari 9, ikiungwa mkono na Ufaransa na washirika mbalimbali nchini humo, utawala huo umekuwa ukijikita katika kujitawala kwa eneo hilo.

Mamlaka ya Mali inaishutumu Ufaransa, nchi ambayo ni mkoloni wa zamani, kwa kuiumia ECOWAS.

Madhumuni ni "kujionyesha kama kigogo, kwa lengo la muda mfupi lisiloeleweka na lisilokubalika la kudhoofisha uchumi ili kuongoza, kwa niaba ya wale tunaowajua, kuharibu na kupindua taasisi za mpito," Alisema Maïga.

Viongozi wa Ufaransa "hawakuwahi kuwaambia raia wao, walipoingilia kati nchini Mali mwaka wa 2013, kwamba wataigawanya nchi hii", aliongeza.

"Hatuwezi kutawaliwa, hatuwezi kuigeuza nchi hii kuwa mtumwa; hayo yamekwisha," alibaini, akimaanisha ukoloni.

Bw. Maïga pia alishambulia Takuba, kundi la kikosi maalum cha Ulaya kilichoanzishwa na Ufaransa na kilichokusudia kuandamana na wanajeshi wa Mali katika mapambano dhidi ya wanajihadi.

Takuba, "ni kugawanya Mali. Ni 'upanga', huko Songhai na Tamasheq, sio jina lililochukuliwa kwa kubahatisha," alisema.

Mbali na kuchelewesha kurejea kwa raia madarakani, Ufaransa na washirika wake wa Ulaya au Marekani wanaituhumu serikali ya kijeshi kwa kuita kundi la mamluki wa Urusi la Wagner, ambalo linaisaidia serikali katika vita vyake.

Mbele ya wanadiplomasia hao, akiwa mstari wa mbele balozi wa Urusi Igor Gromyko, Bw. Maïga aliwafananisha askari wa Jeshi la Kigeni, kikosi cha jeshi la Ufaransa, na mamluki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.