Pata taarifa kuu
ANGOLA-HAKI

Mshirika wa karibu wa rais wa zamani wa Angola dos Santos aweka jela kwa ufisadi

Mfanyabiashara mkubwa nchini Angola, Carlos Manuel de São Vicente, ambaye ni mshirika wa karibu na rais wa zamani dos Santos amehukumiwa na mahakama ya Luanda kifungo cha miaka tisa jela katika kesi kubwa ya rushwa inayojulikana kama "dola milioni 900", kulingana na redio ya taifa Ijumaa.

Tangu aingie madarakani mwaka wa 2017, Rais wa sasa João Lourenço ameanzisha kampeni ya kurejesha mabilioni yanayodaiwa kuwa yamefujwa chini ya uongozi wa muda mrefu wa mtangulizi wake.
Tangu aingie madarakani mwaka wa 2017, Rais wa sasa João Lourenço ameanzisha kampeni ya kurejesha mabilioni yanayodaiwa kuwa yamefujwa chini ya uongozi wa muda mrefu wa mtangulizi wake. AFP - OSVALDO SILVA
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi, Carlos Manuel de São Vicente alipatikana na hatia ya ubadhirifu, utakatishaji fedha na kukwepa kulipa kodi. Amepata moja ya hukumu kubwa zaidi iliyotolewa kwa ufisadi katika nchi hii.

Carlos Manuel de São Vicente ambaye ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bima ya AAA Seguros, tangu ilipovunjwa, alishutumiwa kuwa alihitimisha kinyume cha sheria kandarasi za bima katika tasnia ya mafuta, hasa kwa kampuni ya umma ya Sonangol, akinufaika kutokana na ushirikiano wa karibu aliokuwa nao na rais wa zamani José Eduardo dos Santos.

Akiwa madarakani kuanzia mwaka 1979 hadi 2017, Bw. dos Santos alituhumiwa kuwanufaisha jamaa zake na wasomi wachache kutokana na utajiri unaotokana na akiba kubwa ya mafuta na madini nchini.

Bw. de São Vicente amekuwa akikanusha kila mara, lakini ukubwa wa ulaghai huo ulishtua nchi ambayo imezoea kuona hazina ya umma ikitwaliwa na ufisadi na upendeleo.

Kesi hiyo ya kashfa pia inafunguliwa nchini Uswisi, ambapo mfanyabiashara huyo anatuhumiwa kuweka mamilioni ya fedha katika benki huko Geneva.

Tangu aingie madarakani mwaka wa 2017, Rais wa sasa João Lourenço ameanzisha kampeni ya kurejesha mabilioni yanayodaiwa kuwa yamefujwa chini ya uongozi wa muda mrefu wa mtangulizi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.