Pata taarifa kuu

Kwa nini Mali inaishutumu Ufaransa kwa kuunga mkono wanajihadi?

Mali inajikuta katika malumbano dhidi ya Ufaransa, wakati huu mbele ya Umoja wa Mataifa. Wakati Ufaransa ilikamilisha zoezi la kuondoa kikosi cha Barkhane mwanzoni mwa wiki hii, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali aliliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akilitaka kukemea ukiukaji wa anga ya Mali. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali, Abdoulaye Diop.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali, Abdoulaye Diop. AFP - BRENDAN SMIALOWSKI
Matangazo ya kibiashara

Abdoulaye Diop pia analishutumu jeshi la Ufaransa kwa kuunga mkono wanajihadi. Taarifa hizo zilifichuliwa na wenzetu kutoka Jeune Afrique, lakini RFI pia iliweza kupata barua hii.

Talataye mnamo Agosti 6, Lerneb mnamo Agosti 7, kati ya Tessit na Gao mnamo Agosti 8. Katika barua yake Abdoulaye Diop anataja mfululizo wa ndege za Ufaransa kupaa kwenye anga ya Mali, ambazo zilitoa msaada kwa kikosi cha Ufaransa cha Barkhane kufuatilia jeshi la Mali, kulitisha na zaidi ya yote "kukusanya taarifa za kijasusi kwa manufaa ya makundi ya kigaidi" na "kuwadondoshea silaha na risasi. "

Visa hamsini vya ukiukwaji wa anga ya Mali

Kwa jumla, Bamako inashutumu kuhusu visa hamsini vya ukiukwaji wa anga yake na ndege zisizo na rubani, helikopta au ndege za kivita za Ufaransa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Shutuma na takwimu ambazo tayari zinajulikana, kwani serikali ya Mali ilikuwa tayari imeziripoti mwishoni mwa mwezi wa Aprili. Wakati huo, Mali na Ufaransa zilishutumu kila mmoja kwa kuhusika na mauaji ya halaiki baada ya kugundulika kwa kaburi la halaiki katika eneio la Gossi. Ufaransa ilishutumu "kampeni ya upotoshaji" iliyoandaliwa na washirika wapya wa Bamako kutoka Urusi.

Kumalizika kwa Operesheni Barkhane nchini Mali ilitangazwa Februari na Ufaransa, na zoezi la kuondoa wanajeshi wake pia lilikamilika mwanzoni mwa wiki hii. Lakini ilikuwa mwezi wa Mei mwaka jana ambapo Mali ilipinga rasmi makubaliano ya ulinzi yanayoifungamanisha na Ufaransa: tangu wakati huo, nchi hizo mbili zimekuwa na maono tofauti ya kile ambacho jeshi la Ufaransa bado lingeweza kufanya kisheria katika ardhi ya Mali.

'Hatua zisizoratibiwa za upande mmoja'

Katika kipindi hiki, Barkhane ilikiri kufanya shughuli za kukabiliana na ugaidi. Bamako inashutumu "vitendo visivyoratibiwa vya upande mmoja" pamoja na Mali na kuomba mkutano wa dharura katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Waziri Diop anatishia "kujihami" mbele ya kile anachoelezea kama "uchokozi. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.