Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

Angola: Unita bado inapinga matokeo ya awali ya Uchaguzi Mkuu

Wakati Angola ilitoa heshima za mwisho Jumapili Agosti 28 kwa rais wake wa zamani José Eduardo dos Santos, nchi hiyo bado inasubiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano Agosti 24. 

"Sisi ni watulivu, tuna idadi yetu ya kura na tunajua kwamba tutapata wabunge zaidi," aliema Adalberto Costa Junior (picha yetu).
"Sisi ni watulivu, tuna idadi yetu ya kura na tunajua kwamba tutapata wabunge zaidi," aliema Adalberto Costa Junior (picha yetu). REUTERS - SIPHIWE SIBEKO
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na matokeo ya awali yaliyotolewa Alhamisi wiki iliyopita na Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi, chama cha Popular Movement for Liberation of Angola (MPLA), cha Rais anayemaliza muda wake Joao Lourenço kinachukuwa nafasi ya kwanza kwa zaidi ya 51% ya kura. Chama kinachofuata ni Unita, kinchongozwa na Adalberto Costa Junior ambacho kilipata zaidi ya 44% tu ya kura. Chama cha Unita kimeendelea na msimamo wake wa kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wakati sherehe za kutoa heshima za mwisho kwa hayati rais Dos Santoszilikuwa zikiendelea jana Jumapili.

"Sisi ni watulivu, tuna idadi yetu ya kura na tunajua kwamba tutapata wabunge zaidi," alisema Adalberto Costa Junior, baada ya mazishi ya José Eduardo dos Santos. Licha ya maadhimisho ya kitaifa, kiongozi wa Unita hajapoteza lengo lake.

Makosa

Tangu Ijumaa, amekuwa akipinga matokeo ya awali yaliyotangazwa na CNE. Jumamosi jioni, wajumbe watano wa Tume hiyo ya uchaguzi, ambayo ina maafisa kumi na sita, walitishia kutothibitisha matokeo ya mwisho, kutokana na makosa ambayo yalidhihirishwa. Wajumbe hawa ni wawakilishi wa vyama vya upinzani ndani ya CNE.

Mivutano

Kupingana kwa matokeo ya uchaguzi kumezua mvutano wikendi hii katika baadhi ya wilaya za Luanda, kama vile Cacuaco au Sambizanga. Hata hivyo, mvutano huo ulidhibitiwa haraka. Sherehe za kotoa heshima za mwisho kwa José Eduardo dos Santos zimewezesha kwa wakati unaofaa mamlaka kupeleka idadi kubwa ya vikosi vya usalama, hasa katikati mwa jiji.

Wanaharakati wa mashirika ya kiraia wameripotiwa kukamatwa kulingana na sirika la kiraia linalopinga matokeo hayo ya Uchaguzi Mkuu, ambalo litazungumzi juu ya suala hilo wakati wa mchana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.