Pata taarifa kuu

Angola: Mwili wa Eduardo dos Santos kukabidhiwa mjane wake na kurejeshwa nyumbani

Mwili wa José Eduardo dos Santos utakabidhiwa kwa mjane wake ili kurejeshwa nyumbani na kuzikwa nchini Angola, mahakama ya Barcelona imeamua katika uamuzi uliofanywa hadharani Jumatano hii, Agosti 17. Hatima ya mwili wa mkuu wa zamani wa nchi ya Angola iko katikati ya vita vya kisheria kati ya mjane wake na mmoja wa binti zake, tangu kifo chake huko Barcelona, ​​Julai 8.

Mnamo 2017, miaka 38 baada ya kula kiapo cha kwanza, Dos Santos aliwashangaza Waangola wengi kwa kujiuzulu.
Mnamo 2017, miaka 38 baada ya kula kiapo cha kwanza, Dos Santos aliwashangaza Waangola wengi kwa kujiuzulu. LUSA - AMPE ROGÉRIO
Matangazo ya kibiashara

José Eduardo dos Santos, rais wa pili wa Angola ambaye alitawala taifa hilo lenye utajiri wa madini kwa takriban miongo minne, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79, serikali inasema.

Alifariki nchini Uhispania ambako alipatiwa matibabu baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo. Dos Santos atakumbukwa kwa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu mwanzoni mwa miaka ya 2000 - wafuasi wake walimwita "mbunifu wa amani".

Lakini urithi wake umechafuliwa na viwango vya juu vya ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu alipokuwa madarakani.

Miaka minne tu baada ya kupata uhuru mwaka 1975, nchi hiyo ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi mawili yaliyokuwa yakipigania ukoloni wa Ureno - MPLA ya Dos Santos na Unita.

Vita hivyo vilidumu kwa miaka 27 na kuangamiza nchi. Takriban watu 500,000 wanaaminika kufariki katika mzozo huo.

Pia ilivutia mataifa ya kigeni, huku Afrika Kusini - wakati huo ikiwa chini ya utawala wa wazungu wachache - kutuma wanajeshi kuunga mkono Unita, wakati vikosi vya Cuba viliingilia kati upande wa serikali. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.