Pata taarifa kuu

Kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi, njaa barani Afrika itaongezeka, UN yaonya

Nchini Misri, maelfu ya wajumbe wanajadili Tabia nchi katika mkutano wa COP27. Ikiwa hakuna kitakachofanyika "haraka", kwa nchi jirani ya Sudan, kama nchi nyingine nyingi zinazoendelea, mafuriko, ukame na majanga ya asili yatasababisha "kuongezeka" kwa njaa, anaonya afisa wa Umoja wa Mataifa.

Somalia inakabiliwa na ukame unaoendelea.
Somalia inakabiliwa na ukame unaoendelea. © AP Photo/Elias Meseret
Matangazo ya kibiashara

Zitouni Ould-Dada, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Hali ya Hewa na Mazingira wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), mkutano wa COP27, "African COP" kama waandaaji wake wanavyodai, lazima iwe fursa ya kurejelea mada ya usalama wa chakula barani humo.

"Siyo kawaida kwamba Afrika inaleta 40% ya ngano yake kutoka Urusi na Ukraine wakati yenyewe ina utajiri wa rasilimali," ameliambia shirika la habari la AFP kando ya mkutano huu wa COP27 huko Sharm el-Sheikh. "Inahitaji utashi wa kisiasa kupambana na umaskini na njaa duniani kote."

'Dharura'

Kwa sababu, anaonya, "ikiwa hatua kali hazitachukuliwa kwa haraka, njaa itaongezeka kwa sababu mabadiliko ya Tabia nchi yanayoonekana kila mahali na hasa katika maeneo hatarishi kama vile Sudan", amethibitisha afisa huyo.

Sudan, ambako joto kali hutawala kwa muda mwingi wa mwaka na mvua kubwa iliyonyesha tena iliua karibu watu 150 msimu huu wa joto, ni nchi ya tano katika hatari zaidi duniani kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi, kulingana na taasisi ya Global Adaptation Index ya Chuo Kikuu cha Marekani cha Notre Damex.

Na nchi hiyo ina rekodi ya kusikitisha: vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo tangu mwaka 2003 vimesababisha vifo vya watu 300,000 na zaidi ya milioni mbili kuyahama makazi yao huko Darfur, kwenye mpaka wa magharibi wa Chad, vimetangazwa na waangalizi kuwa vita vya "kwanza" vya dunia vinavyohusishwa na mabadiliko ya Tabia nchi.

Tangu wakati huo, migogoro ya kikabila kuhusu mifugo au upatikanaji wa maji na malisho inaendelea kusababisha mamia ya vifo kila mwaka: zaidi ya vifo 800 tangu mwezi wa Januari, kulingana na Umoja wa Mataifa, na zaidi ya watu 260,000 wamekimbia makazi yao.

Leo, katika nchi ambayo tayari inakabiliwa na mfumuko wa bei na kukatizwa kwa misaada ya kimataifa baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka mmoja uliopita, wakazi 15 kati ya milioni 45 wanakabiliwa na njaa, 50% zaidi kuliko mwaka wa 2021, kulingana na shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.