Pata taarifa kuu

Siku ya kupiga kura nchini Equatorial Guinea: Rais Obiang awania muhula wa 6

Akiwa na umri wa miaka 80, Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo amekuwa madarakani tangu 1979. Katika chaguzi zilizopita, alipata kura zaidi ya 93%.

Mabango yenye picha za Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, mjini Malabo tarehe 17 Novemba 2022.
Mabango yenye picha za Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, mjini Malabo tarehe 17 Novemba 2022. © AFP - SAMUEL OBIANG
Matangazo ya kibiashara

Equatorial Guinea inamchagua rais, wabunge na maseneta wake siku ya Jumapili, ushindi wa Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, aliyetawala kwa miaka 43, hauna ma shaka mbele ya upinzani uliozimishwa.

Kwa jumla, raia 427,661 walio na umri wa kupiga kura kati ya wakaazi milioni 1.4 wameitwa kupiga kura. Matokeo ya kura hizi za duru moja yanatarajiwa kutangazwa Jumatatu kwa uchaguzi wa urais, labda baadaye kwa chaguzi zingine.

Akiwania muhula wa sita akiwa na umri wa miaka 80, Bw. Obiang anashikilia rekodi ya dunia ya kuishi muda mrefu madarakani kama rais, nje ya utawala wa kifalme.

Daima amechaguliwa kwa zaidi ya 93% ya kura na chama chake chenye nguvu zaidi cha Democratic Equatorial Guinea (PDGE) ambacho kinashikilia viti 99 kati ya 100 katika Baraza la wawakilishi linalomaliza muda wake na 55 katika Bunge la Seneti.

Wapinzani wawili katika mbio hizi za urais

Ili kuwania muhula mpya wa miaka saba, Teodoro Obiang anakabiliwa na wagombea wawili: Andrès Esono Ondo, mgombea wa Convergence for Social Democracy (CPDS), chama pekee cha upinzani ambacho hakijapigwa marufuku, na Buenaventura Monsuy Asumu wa Coalition Party Social Democrat. (PCSD), chama kidogo ambacho hadi sasa kinashirikiana na PDGE katika uchaguzi wa wabunge.

Mkuu wa nchi alichukua mamlaka katika mapinduzi mwaka 1979 katika nchi hii ya mafuta ya Afrika ya Kati iliyopata uhuru kutoka Uhispania tangu 1968.

Utawala wake mara kwa mara unashutumiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa na miji mikuu ya Magharibi kwa kukandamiza upinzani wote na kukiuka haki za binadamu, na kulaumiwa kwa ufisadi uliokithiri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.