Pata taarifa kuu

DRC: Mkutano mdogo kuhusu mgogogoro mashariki mwa DRC kufanyika kati ya Kinshasa na Kigali

Wakati hali ya utulivu ikitawala tena tangu Novemba 22 katika mjoa wa Kivu Kaskazini, wakuu kadhaa wa nchi kutoka eneo la Maziwa Makuu wako Luanda Jumatano hii, Novemba 23 kujadili hali ya mashariki mwa DRC.

Waasi wa M23 mashariki mwa DRC.
Waasi wa M23 mashariki mwa DRC. © REUTERS - James Akena
Matangazo ya kibiashara

Felix Tshisekedi na Paul Kagame wanatarajiwa katika mji mkuu wa Angola. Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye na mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na mwezeshaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, Uhuru Kenyatta pia wapo katika mji mkuu wa Angola, Luanda. Lengo kuu la mkutano huu mdogo ni kufanya kazi kwa lengo la kukomesha uhasama kati ya Kinshasa na Kigali.

Kinachotakiwa kufanyika

Joao Lourenço amekuwa akishughulikia suala hili tangu mwezi Julai 2022: aliandaa mkutano kati ya Tshisekedi na Kagame. Na kilichotakiwa kufuatwa kilikuwa kimeandaliwa, lakini hakikutumika. Mpatanishi aliyeteuliwa na Umoja wa Afrika (AU), rais wa Angola alikuwa amejihusisha na kampeni zake za kuchaguliwa tena hadi mwisho wa mwezi wa Agosti. Leo, anataka kutekeleza mpango wake kwenye meza ya mazungumzo, katika toleo lililosasishwa.

Kuweka sawa ajenda za Luanda na Nairobi

Majadiliano mapya lazima yafanyike na makundi yenye silaha mashariki mwa DRC. Miadi iliyoahirishwa mara kadhaa sasa imepangwa Novemba 27. Lakini Rwanda inasubiri kuona kitakachofanywa. Mwishoni mwa juma lililopita, Paul Kagame aliahidi Uhuru Kenyatta "kuwahimiza M23 kusitisha mapigano na kujiondoa kutoka kwa maeneo yaliyotekwa"; mapigano yalianza tena katika mkoa wa Kivu Kaskazini tarehe 20 Novemba. Kulinagana na vyanzo kutoka DRC, waasi wanataka kuwa na wawe na sauti, hasa kuhusu kuingizwa katika vikosi vya usalama na jeshi. Lakini serikali ya DRC inaendelea kupinga jambo hilo: Kinshasa kamwe haitokubali kufanya mazungumzo na M23.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.