Pata taarifa kuu
ETHIOPIA- USALAMA.

Wapatanishi wa mzozo nchini Ethiopia wamezuru Mekelle kwa mara ya kwanza

Wasuluhishi wa mzozo kati ya serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray, jana walitembelea mji wa Mekelle kwa mara ya kwanza, tangu pande mbili zilipotia saini mkataba wa amani mwezi uliopita jijini Pretoria.

Ethiopian government representative Redwan Hussien and Tigray delegate Getachew Reda attend signing of the AU-led negotiations to resolve the conflict in northern Ethiopia, in Pretoria, South Africa, 2 November 2022.
Ethiopian government representative Redwan Hussien and Tigray delegate Getachew Reda attend signing of the AU-led negotiations to resolve the conflict in northern Ethiopia, in Pretoria, South Africa, 2 November 2022. © Siphiwe Sibeko/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wakiongozwa na wasuluhishi kutoka Umoja wa Afrika, marais wa zamani Uhuru Kenyatta na Olusegun Obansanjo wameugana na wajumbe wengine zaidi ya 30 kutoka Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya, ili kuthathmini utekelezwaji wa makubaliano kati ya pande mbili.

Getachew Reda, mshauri wa kiongozi wa waasi wa Tigray anasema hatua inayofanyika ni muhimu.

“Tukiweka vichwa vyetu pamoja, hakuna tusichoweza kufanya, tunashukuru hatua ambayo imepigwa mpaka sasa ila bado tuna kazi kubw ana safari ndefu.” Amesema Getachew Reda.

Mapigano ya miaka mwili kati ya wapiganaji wa Tigray na serikali ya shirikisho ya Ethiopia yamesababisha idadi kubwa ya raia kuyakimbia makazi yao kwa hofu ya kushambuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.