Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

DRC: Uhuru Kenyatta atoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mapya

Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ambaye pia ni mpatanishi katika mzozo wa usalama mashariki mwa DRC, hapo jana ametoa mwito wa kusitishwa kwa machafuko yaliyozuka tangu mwishoni mwa juma lililopita.

Uhuru Kenyatta, Rais wa zamani wa Kenya
Uhuru Kenyatta, Rais wa zamani wa Kenya © Monicah Mwangi / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kenyatta ambaye anasuluhisha mzozo huo kwa niaba ya jumuiya ya Afrika Mashariki, kupitia taarifa yake, ameeleza kuguswa na ripoti za mapigano na mauaji ya kiholela ya raia kwenye eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa ya ofisi yake imeongeza kuwa, mpatanishi anaguswa na mauaji ya raia yanayotekelezwa na makundi yenye silaha, hali iliyosababisha maelfu ya raia kukimbia nyumba zao katika muda wa siku mbili peke yake.

Kauli ya Uhuru Kenyatta, imekuja saa chache tangu serikali ya DRC na Rwanda zirushiane maneno, Kinshasa ikiituhumu Kigali kwa uchokozi baada ya kushambulia ndege yake ya kivita kwenye eneo la Goma.

Licha ya taarifa ya Kenyatta kutotaja moja kwa moja tukio la kushambuliwa ndege ya DRC, amezitaka pande zinazohusika kwenye mgogoro ulioko kuendelea kuheshimu makubaliano ya Luanda Angola na Nairobi.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.