Pata taarifa kuu

Misri: Mkuu wa zamani wa kitengo cha kupambana na ufisadi aachiliwa na kufunguliwa mashitaka tena

Rais wa zamani wa kitengo cha  Kupambana dhidi ya ufisadi nchini Misri, Hicham Geneina, aliachiliwa huru siku ya Jumanne baada ya miaka mitano jela kwa "ugaidi" na "taarifa za uwongo", kisha kufunguliwa mashitaka yale yale na mahakama nyingine, mwanaharakati wa haki za binadamu ameliambia shirika la habari la AFP.

Hicham Geneina, mwenyekiti wa zamani wa Mamlaka ya Kupambana na Rushwa nchini Misri, Juni 23, 2016, mjini Cairo.
Hicham Geneina, mwenyekiti wa zamani wa Mamlaka ya Kupambana na Rushwa nchini Misri, Juni 23, 2016, mjini Cairo. KHALED DESOUKI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Bw Geneina, aliyekamatwa mwaka wa 2018 alipokuwa akimfanyia kampeni Sami Anan, mpinzani wa rais wa Abdel Fattah al-Sissi, alihukumiwa na mahakama ya kijeshi baada ya mahojiano ambapo alipendekeza kuwepo kwa nyaraka za siri zinazoathiri watawala wa Misri.

Jumanne, wakati wa kuachiliwa kwake kutoka gerezani, mwanaharakati huyo aliwasilishwa kwa mwendesha mashtaka wa kiraia wa Usalama wa Nchi ambaye "alimwachilia bila dhamana lakini kwa sharti la kutoa anwani yake", Hossam Bahgat ameliambia shirika la habari la  AFP.

Hii ina maana kwamba anaweza kuitwa tena kuhojiwa wakati wowote kwa sababu "sasa anafunguliwa mashitaka katika kesi nyingine inayosimamiwa na mashtaka ya kiraia ya Usalama wa Serikali", ya 2018, ameongeza.

Kwa upande wa mwanaharakati, anasema mashtaka haya mapya ni "ya kawaida ya mfumo wa mzunguko", ujanja unaotumika, kulingana na watetezi wa haki za binadamu, kuwaweka wapinzani gerezani au katika ardhi ya Misri zaidi ya muda uliowekwa kisheria.

Mnamo 2016, Bw. Geneina alifutwa kazi na Bw. Sissi, aliyechaguliwa kuwa rais mwaka wa 2014 kisha akachaguliwa tena mwaka wa 2018, na kushutumiwa kwa "taarifa za uwongo" kwa kukadiria ufisadi wa umma kati ya 2012 na 2015 kwa euro bilioni 60.

Siku ya Jumatatu, kiongozi mwingine wa upinzani, Mamdouh Hamza, aliweza kurejea Misri baada ya mahakama mwaka 2021 kuamuru kuondolewa kwa jina lake kwenye orodha ya marufuku kufika uwanja wa ndege wa Cairo.

Mamdouh Hamza aliwekwa kwenye orodha hii baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani kwa "ugaidi", kwa kuonyesha kwenye Twitter, mwaka wa 2017, msaada wake kwa wakazi wa Cairo ulitishia kufukuzwa kwa manufaa ya miradi ya mali isiyohamishika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.