Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-ULINZI

DRC: Kikosi cha Angola kusaidia operesheni za kulinda amani

Ukosefu wa usalama mashariki mwa DRC: Angola itatuma kikosi kusaidia shughuli za ulinzi wa amani. Ofisi ya rais wa Angola ilitangaza hilo jana, Jumamosi, Machi 11, katika taarifa yake. Kulingana na Luanda, uamuzi huu ulichukuliwa baada ya mashauriano na Kinshasa; Umoja wa Mataifa na viongozi wengine katika ukanda huo wamefahamishwa kuhusu mpango huu.

Watoto wakicheza kwenye kifaru kilichotelekezwa na M23 katika eneo la Goma. jukumu la wanajeshi wa Angola: kulinda maeneo watakakokusanywa waasi wa M23 na kuwalinda wajumbe wa timu yenye jukumu la kufuatilia usitishaji mapigano.
Watoto wakicheza kwenye kifaru kilichotelekezwa na M23 katika eneo la Goma. jukumu la wanajeshi wa Angola: kulinda maeneo watakakokusanywa waasi wa M23 na kuwalinda wajumbe wa timu yenye jukumu la kufuatilia usitishaji mapigano. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Kamanda wa Kamanda Muzembe

Kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye akaunti ya Facebook ya ofisi ya rais wa Angola, dhamira kuu ya kitengo hiki itakuwa kulinda maeneo watakapokusanywa waasi wa M23 na kuwalinda wajumbe wa timu itakayohusika na ufuatiliaji wa  usitishaji mapigano. Hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kuhusu idadi ya wanajeshi wa Angola ambao watatumwa mashariki mwa DRC.

Kilichomo

Mpango huo ni sehemu ya mikutano mbalimbali kuhusu mchakato wa amani na usalama, mikutano ambayo Luanda ina jukumu kama mpatanishi. Mnamo mwezi Julai 2022, wakati wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya nchi za Maziwa Makuu, ICGLR, afisa mkuu wa Angola aliteuliwa kusimamia tume ya mseto ya uchunguzi. Tume itakayochunguza tuhuma za pande mbili kati ya DRC na Rwanda pamoja na madai ya ukiukaji wa mpaka kati ya majirani hao wawili.

Wataalam

Mfumo huu pia unajumuisha timu ya wataalam watatu wa Angola walioko katika jiji la Goma, na kuungwa mkono na tume ya pamoja ya mseto ya uchunguzi ya ICGLR na MONUSCO. Kutumwa kwa wanajeshi hao wa Angola bado kunahitaji kuidhinishwa na bunge la Angola. Hii si mara ya kwanza kwa Angola kuingilia kati nchini DRC. Katika miaka ya 1997, Luanda iliingilia kati kumsaidia Rais Laurent-Désiré Kabila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.