Pata taarifa kuu

DRC: Wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wazuru Goma

NAIROBI – Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja umetembelea mji wa Goma, kuthathmini hali ya usalama na kibinadamu jimboni Kivu Kaskazini, wakati huu mapigano yakiendelea kushuhudiwa kati ya waasi wa M 23 na wanajeshi wa serikali. 

Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja umezuru mji wa Goma, kuthathmini hali ya usalama na kibinadamu jimboni Kivu Kaskazini
Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja umezuru mji wa Goma, kuthathmini hali ya usalama na kibinadamu jimboni Kivu Kaskazini Photo MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

Mwandishi wetu wa Goma Chube Ngorombi, amaezungumza na baadhi ya wakaazi wa Goma kuhusu matarajio ya ziara hiyo. 

 “Ziara yao haina maana ila inaweza kuwa na maana kwa sababu wakitoka huku tutapata amani, hiyo inaonyesha kuwa umoja wa mataifa uko pamoja na raia wa Congo. ”wamesema baadhi ya raia wa Goma.

Siku ya Ijuma ya wiki hii wajumbe hao walikutana na kufanya mazungumzo na rais Tshisekedi jijini Kinshasa, ambaye alitumia fursa hiyo kuendelea kusisitiza kuwa Rwanda inawaunga mkono waasi M 23 na kutaka nchi hiyo kuwekewa vikwazo. 

 Hata hivyo, madai ya Tshisekedi ameendelea kukanushwa na rais wa Rwanda, Paul Kagame. 

Rais João Lourenço ambaye nchi yake ni msuluhishi wa ukanda mzozo huo, amesema kikosi cha nchi yake kitatumwa katika maeneo ambayo kuna waasi wa M 23 kwa lengo la kuwalinda raia, na kuhakikisha kuwa mkataba usitishwaji wa vita, unatekelezwa. 

 Hatua ya Angola ikija wakati huu waasi M 23 katika taarifa yao waliyoitoa leo, wamekitaka kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kuchukua udhibiti wa vijiji vya Karuba, Muremure, Nyamitima, Nkingo, Kagano na Kihuli, ambavyo wamekuwa wakidhibiti. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.