Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa Maseneta nchini Cameroon: Chama tawala chapewa nafasi kubwa ya kushinda

Chama cha RDPC cha Rais Paul Biya, ambaye ametawala Cameroon kwa zaidi ya miaka 40, kinatarajiwa kushinda kwa urahisi uchaguzi wa maseneta ambao ulianza Jumapili asubuhi kwa kura isiyo ya moja kwa moja. Chama tawala cha RDPC, kinadhibiti manispaa 316 kati ya 360 nchini Cameroon.

Mwanajeshi wa Cameroon akiwa amesimama nje ya kituo cha kupigia kura mjini Yaoundé wakati wa uchaguzi wa urais wa Oktoba 9, 2011 nchini Cameroon.
Mwanajeshi wa Cameroon akiwa amesimama nje ya kituo cha kupigia kura mjini Yaoundé wakati wa uchaguzi wa urais wa Oktoba 9, 2011 nchini Cameroon. ASSOCIATED PRESS - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Kura ilianza saa mbili asubuhi katika vituo sita vya kupigia kura huko Yaoundé, vilivyowekwa katika shule ya umma ya Bastos, wilaya ya juu zaidi ya mji mkuu, ambapo hapakuwa na umati wa watu saa za mapema, ameshuhudia mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

Katika mikoa kumi ya kiutawala ya nchi hii ya Afrika ya Kati yenye wakazi wapatao milioni 28, vyama 10 vimewasilisha wagombea kwa wapiga kura 11,134: madiwani wa mikoa, madiwani wa manispaa na machifu wa kimila.

Lakini caham cha RDPC ndicho pekee kilichowasilisha orodha ya wagombea wake katika mikoa yote kumi na kinadhibiti wilaya 316 kati ya 360 nchini Cameroon.

Bunge la Seneti linatawaliwa na mamlaka. Maseneta 70 huchaguliwa kila baada ya miaka mitano na 30 huteuliwa na Rais wa Jamhuri. Katika Bunge la Seneti linalo maliza muda wake, chama cha RDPC na washirika wake wadogo wanakalia viti 93 kati ya 100, saba vilivyosalia vikienda kwa chama cha Social Democratic Front (SDF), mojawapo ya vyama viwili vikuu vya upinzani.

Katika Baraza la Bunge, chama cha Bw. Biya na washirika wake pia wana idadi kubwa ya wabunge 164 kati ya 180, waliochaguliwa moja kwa moja mnamo mwezi Februari 2020.

"Chama cha RDPC kinapewa nafasi kubwa ya kushinda leo Jumapili, kwa sababu wanachama wake ndio wengi zaidi katika Bodi ya Uchaguzi", Louison Essomba, profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Douala, ameliahakikidhia shirika la habarila AFP, huku akitabiri "wingi wa kupindukia wa wabunge".

"Sioni changamoto yoyote, hata umuhimu wa Bunge hili la Seneti", anasema Serge Dzou, profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Ngaoundéré (kaskazini), huku akiongeza  Bunge hili la Seneti "linatumika tu kutoa nafasi kwa wale walio karibu na utawala".

Paul Biya ameitawala Cameroon tangu mwaka 1982, akishutumiwa mara kwa mara na Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa kwa kukandamiza kikatili upinzani mitaani na waasi wanaotaka kujitenga kwamikoa miwili ya magharibi inayokaliwa zaidi na watu wachache wanaozungumza Kiingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.