Pata taarifa kuu

Ethiopia: Serikali kuaanza majadiliano na kundi la waasi wa Oromo Liberation Army (OLA)

NAIROBI – Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, hapo jana Jumapili katika hafla ya kusherehekea makubaliano ya amani yalioafikiwa kati ya serikali na vikosi vya Tigray, amesema kwamba juma hili, serikali yake itaanzisha majadiliano na kundi la waasi wa Oromo Liberation Army (OLA) nchini Tanzania.

Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta ametuzwa kwa juhudi zake za kuleta amani nchini Ethiopia
Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta ametuzwa kwa juhudi zake za kuleta amani nchini Ethiopia © office of the fourth president of Kenya
Matangazo ya kibiashara

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa serikali ya Abiy kutangaza rasmi majadiliano na waasi hao ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilaumiana na serikali juu ya mashambulio katika eneo la Oromia

OLA ni kundi lililopigwa marufuku la Oromo Liberation Front, chama cha upinzani kilichopigwa marufuku hapo awali ambacho kilirejea kutoka uhamishoni baada ya Abiy kuchukua madaraka mwaka wa 2018.

Malalamiko ya kundi hilo yanatokana na madai ya kutengwa kwa watu wa Oromo na kupuuzwa na serikali ya shirikisho.

OLA na serikali ya shirikisho zinalaumiana kwa mashambulizi kadhaa katika eneo la Oromia nchini Ethiopia, lenye wakazi wengi zaidi nchini humo, ambapo raia wengi wameuawa.

Uhuru Kenyatta ni rais mstaafu wa Kenya na mmoja wa wapatanishi wa mzozo wa Tigray, ni miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo.

“Ethiopia ni nchi ambayo imekuwa kielelezo barani Afrika kwa kuonyesha namna raia wan chi tofauti na jamii tofauti wanaweza kuishi pamoja kwa amani.”alisema rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta.

00:35

Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta kuhusu Ethiopia

Aidha kiongozi huyo wa zamani wa Kenya alisema kuwa uongozi wa Umoja wa Afrika umedhihirisha kwamba Afrika inaweza kutatua chanagmoto zake kwa kupitia usuluhisaji wa ndani ya bara Afrika.

Kenyatta alituzwa kutokana na juhudi zake za upatikanaji wa amani nchini Ethiopia wakati wa halfa hiyo.

Makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano nchini Ethiopia kati ya wanajeshi wa serikali na wapganaji wa TPLF yalimaliza vita vya karibia miaka miwili katika taifa hilo, mamia ya watu wakiripotiwa kufariki wakati maelfu ya wengine wakiripotiwa kutoroka kwa kuhofia kushambuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.