DRC: Salomon Idi Kalonda, mshauri maalum wa Moïse Katumbi akamatwa
Hali ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inazidi kuwa ngumu miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu. Mnamo Mei 30, 2023, katika mji mkuu Kinshasa, mwanasiasa wa upinzani Salomon Idi Kalonda, mshauri maalum wa Moïse Katumbi, aliyetangazwa kuwa mgombea wa uchaguzi ujao wa urais, amekamatwa na idara za ujasusi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa N'djili alipokuwa akijiandaa kuondoka Kinshasa na kiongozi wake.
Imechapishwa:
Upinzani na mashirika ya kiraia yamelaani kitendo hicho huku Moïse Katumbi anazungumzia kitendo hicho kuwa ni utekaji nyara "mbaya"; ni demokrasia ambayo 'imeangamizwa', anasema Waziri Mkuu wa zamani Matata Ponyo; Georges Kapiamba, kutoka mashirika ya kiraia, anaomba kuachiliwa kwake mara moja.
Mamlaka bado haijatoa taarifa yoyote kuhusu sababu za kukamatwa kwa mwanasiasa huyo wa upinzani.