Pata taarifa kuu

DRC : CENI yaanza zoezi la ukaguzi wa daftari la wapiga kura

NAIROBI – Tume ya taifa ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeanzisha utaratibu wa kufanya ukaguzi wa daftari la wapiga kura kwa kutumia maafisa kadhaa wa taasisi za nje kuelekea uchaguzi wa disemba mwaka huu.

Tume ya taifa ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeanzisha utaratibu wa kufanya ukaguzi wa daftari la wapiga
Tume ya taifa ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeanzisha utaratibu wa kufanya ukaguzi wa daftari la wapiga © John Wessels - AFP
Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kuwaandika wapigakura lilitamatika  mwezi wa Aprili, licha ya kuwa sehemu kadhaa kama maeneo ya Rutshuru na Masisi mkowani Kivu kaskazini upande wa mashariki, eneo la Maluku kule Kinshasa na Kwamouth upande wa magharibi raia wengi hawakushiriki zoezi hilo kutokana na sababu za kiusalama.

Baadhi ya wanasiasa wamehoji kuhusu aina ya uchaguzi unaokwenda kufanyika katika nchi hiyo, wakati idadi kubwa ya wananchi wamekabiliwa na tatizo la kiusalama.

Mbali na suala hilo kumekuwa na tatizo la kuwateuwa wataalamu wa kimataifa kutoka nje ya taifa hilo ambao watapewa jukumu la kukagua daftari la wapigakura, baada ya mashirika ya kiraia na wadau wengine kuhoji kuhudu muda unaotakiwa kikatiba kukamilisha zoezi hilo;

Tayari wanasiasa wa upinzani wakiongozwa na Moise Katumbi na Martin Fayulu wanapinga utaratibu ulioanzishwa na CENI kufanya ukaguzi wa nje wa daftari la uchaguzi.

Kituo cha uchaguzi kinasema kimepokea takriban faili mia mbili kutoka kwa wagombeaji wa jukumu hili baada ya Shirika la Kimataifa la La Francophonie (OIF) kukataa jukumu hilo kufuatia muda mfupi wa mwisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.