Pata taarifa kuu

Libya: Siku sita baada ya mafuriko, hali bado ni tete

Nchini Libya, siku sita baada ya mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Daniel, mashariki mwa nchi hiyo, zoezi la utafutaji linaendelea lakini matumaini ya kupata manusura yanazidi kupungua. Kambi ya Marshal Haftar ilizungumza juu ya hali hiyo jioni ya Ijumaa, Septemba 15.

Mji wa Derna ulioatiriwa na maji, mashariki mwa Libya, Septemba 11, 2023.
Mji wa Derna ulioatiriwa na maji, mashariki mwa Libya, Septemba 11, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Marshal Haftar ambaye amezungumza na kubaini juu ya mahitaji makubwa ya ujenzi upya. Mpiga picha wa shirika la habari la AFP anakumbusha matukio ya ukiwa huko Derna: majengo yalisombwa na maji au hata magari yaliharibiwa na kuta. Huko Al Bayda, takriban kilomita mia moja, wakaazi husafisha vilima vya matope, kwenye nyumba na barabarani.

Siku sita baada ya mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Daniel, shughuli za utafutaji na uokoaji zinaendelea. Idadi ya vifo inatofautiana kulingana na chanzo kimoja, lakini inasimama kwa zaidi ya vifo 3,000. Umoja wa Mataifa pia unataja angalau watu 10,000 hawajulikani waliko. Kulingana na Waziri wa Afya wa serikali ya Mashariki, karibu miili mia moja iligunduliwa na kuzikwa siku ya Ijumaa. Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) pia linaripoti watu 38,000 waliokimbia makazi yao. Mashirika kadhaa ya kibinadamu yanaonya juu ya hatari za ugonjwa zinazohusishwa na uwezekano wa uchafuzi wa maji.

Jumamosi hii, Septemba 16, ndege ya tatu ya Ufaransa ilikuwa iondoke ili kuleta vifaa vingine vilivyokusudiwa kusakinishwa hospitali. Shirika lisilo la kiserikali la Madaktari Wasio na Mipaka linaelezea hali ya mbaya na kutoa wito wa uratibu wa haraka wa misaada. Hali ya kisiasa, pamoja na serikali mbili zinazohasimiana – moja mjini Tripoli na nyingine Mashariki – inaonekana kutatiza kazi ya timu hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.