Pata taarifa kuu

Mafuriko nchini Libya: Idadi ya vifo Derna yaongezeka hadi 11,300

Mafuriko yaliyosababishwa wiki iliyopita nchini Libya na kimbunga Daniel yaliua watu 11,300 katika mji wa Derna, kulingana na ripoti mpya iliyochapishwa siku ya Jumamosi jioni na shirika la Umoja wa Mataifa, likinukuu shirika la Hilali Nyekundu nchini Libya. 

Zaidi watu elfu kumi na mmoja wameripotiwa kufariki katika mafuriko hayo
Zaidi watu elfu kumi na mmoja wameripotiwa kufariki katika mafuriko hayo AP - Yousef Murad
Matangazo ya kibiashara

"Kulingana na shirika la Hilali Nyekundu la Libya, mafuriko haya ambayo hayajawahi kutokea yalisababisha vifo vya watu 11,300 na wengine 10,100 kutoweka katika mji wa Derna pekee," ilitangaza Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA). Takriban watu 170 pia walifariki katika maeneo mengine mashariki mwa Libya, Ocha imeongeza. "Idadi hii inatarajiwa kuongezeka wakati timu za utafutaji na uokoaji zikifanya kazi usiku na mchana," shirika la Umoja wa Mataifa limeonya.

Takriban watu 10,100 bado hawajulikani walipo huko Derna, nchini Libya, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema. Janga hilo pia lilisababisha vifo vya watu 170 katika maeneo mengine mashariki mwa Libya, OCHA imeongeza.

Kimbunga Daniel kilipiga mji wa Derna, wenye wakazi 100,000, usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu Septemba 11. Hali hiyo ilisababisha kupasuka kwa mabwawa mawili ya maji ya mto, na kusababisha mafuriko ya ukubwa wa tsunami. Maji hayo yalisomba kila kitu na kusababisha vifo vya maelfu ya watu. Makumi ya miili hutolewa nje na kuzikwa kila siku.

Waziri wa Afya wa utawala wa mashariki mwa Libya alitangaza idadi ya vifo vya watu 3,252 Jumamosi jioni. Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema hapo awali kwamba miili ya watu 3,958 ilipatikana na kutambuliwa, na kwamba "zaidi ya watu 9,000" bado hawajapatikana. Kulingana na shuhuda za wakaazi, wengi wa waathiriwa walikwama chini ya matope au kusombwa hadi katika Bahari ya Mediterania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.