Pata taarifa kuu

Libya : Shughuli ya kutafuta miili ya manusura wa mafuriko inaendelea

Nairobi – Juma moja baada ya Libya kushuhudia mafuriko makubwa ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya watu elfu 3, mashirika ya kimataifa ya misaada yanaendelea kupambana kutafuta miili ya watu ambao bado hawajapatikana hadi sasa na wale ambao huenda walinusurika.

Kando na mashirika ya kimsaada, raia pia wanachangia katika shughuli hizo za uokoaji na upekuzi
Kando na mashirika ya kimsaada, raia pia wanachangia katika shughuli hizo za uokoaji na upekuzi AP - Yousef Murad
Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya umoja ya mataifa yamesema kuna raia zaidi ya elfu thelathini wasio na makazi na wanahitaji wa maji, chakula na msaada wa kimsingi, hali hii ikiwaweka hatari ya kuambukizwa magonjwa kama kipindu pindu, kukosa lishe na kupata utapia mlo au kukosa maji mwilini.

Kando na mashirika ya kimsaada, raia pia wanachangia katika shughuli hizo za uokoaji na upekuzi, wengi wakisema katika kila mji,kila família imeathirika.

Waziri wa afya wa serikali ya Umoja, mashariki mwa Libya,Othman Abdeljalil amesema watu elfu tatu mia mbili hamsini na wawili wamethibitisha kufarika Derna.

Ofisi inayoratibu huduma za msaada katika umoja wa mataifa nako imesema kuwa watu elfi 11 300 wamepoteza maisha.

Mashirika hayo ya misaada na mamlaka nchini humo yamekiri kuna maelfu ya watu ambao bado hawajapatikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.