Pata taarifa kuu

Libya: Wakaazi walioathiriwa na mafuriko mjini Derna wameandamana

Mamia ya wakaazi wa Derna nchini Libya, ulioathiriwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya Elfu tatu na kuwaacha maelfu bila makaazi, wameandamana, kulishtumu Bunge Mashariki mwa nchi hiyo na kutaka wale wote ambao hawakuajibika kuzuia janga hilo kuajibishwa.

Pia walidai fidia, uchunguzi juu ya fedha za jiji na ujenzi wa Derna
Pia walidai fidia, uchunguzi juu ya fedha za jiji na ujenzi wa Derna AFP - ABU BAKR AL-SOUSSI
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji hao wametuhumu kiongozi wa bunge la eneo la mashariki Aguila Saleh,na mamlaka kwenye eneo hilo kwa kutowajibikia mafuriko hayo ambayo yamesababisha vifo vya karibia watu elfu nne kwa mujibu wa takwimu za umoja wa mataifa.

Katika taarifa ya pamoja, waandamanaji hao walisema wanataka uchunguzi wa haraka kufanyika kuhusu janaga hilo na sheria kuchukuliwa dhidi ya viongozi watepetevu.

Pia walidai fidia, uchunguzi juu ya fedha za jiji na ujenzi wa Derna.

Wataalamu pia wamesema hali ya kutoshugulikiwa kwa mabwawa ya jiji hilo na mamlaka kulisababisha kupasuka kwa mabwawa na kutoa maji ya mafuriko
Wataalamu pia wamesema hali ya kutoshugulikiwa kwa mabwawa ya jiji hilo na mamlaka kulisababisha kupasuka kwa mabwawa na kutoa maji ya mafuriko AP - Yousef Murad

Katika hatua nyingine, wiki moja baada ya janga hilo juhudi zinafanyika ili kuepuka kusambaa kwa magonjwa ya mlipuko.

Najwa Mekki ni msemaji kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya misaada ya binadamu OCHA.

“Kipau mbele kwa sasa ni kujaribu kuokoa maisha na kuhakiksha hakuna maradhi nchini, tunafahamu kwamba hatari ya kuambukizwa kwa maji ya kunywa iko juu sana.” alisema Najwa Mekki msemaji kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya misaada ya binadamu OCHA

Mashariki mwa Libya inatawaliwa na serikali tofauti na ile inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa yenye makao yake makuu katika mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Wataalamu kadhaa na mashirika ya kibinadamu yamependekeza kuwa mafuriko yangeweza kudhibitiwa kwa sehemu kubwa iwapo mamlaka za mitaa zingewahamisha wakazi au angalau kuwasilisha maonyo kuhusu kimbunga Daniel.

Zaidi watu elfu kumi na nane wameripotiwa kufariki katika mafuriko hayo kwa mujibu wa takwimu za UN
Zaidi watu elfu kumi na nane wameripotiwa kufariki katika mafuriko hayo kwa mujibu wa takwimu za UN AP - Yousef Murad

Wataalamu pia wamesema hali ya kutoshugulikiwa kwa mabwawa ya jiji hilo na mamlaka kulisababisha kupasuka kwa mabwawa na kutoa maji ya mafuriko.

Waandamanaji pia walichoma nyumba ya meya wa Derna, Abdulmenam al-Ghaithi.

Ghaithi, pamoja na maafisa wengine wa manispaa ya Derna, wamesimamishwa kazi na waziri mkuu wa mashariki mwa Libya Osama Hammad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.