Pata taarifa kuu

Misri: Watu 38 wajeruhiwa baada ya moto kuzuka katika jengo moja Ismailia

Takriban watu 38 wamejeruhiwa katika kisa cha moto ulioteketeza moja ya majengo makubwa katika mji wa Ismailia nchini Misri, kwenye ukingo wa magharibi wa mfereji wa Suez leo Jumatatu. Moto huo ambao chanzo chake bado hakijajulikana, ulizuka katika makao makuu ya Kurugenzi ya Usalama kabla ya alfajiri.

Wizara ya Afya imetuma ambulensi 50 kwenye eneo la tukio, pamoja na maafisa wa idara ya huduma za dharura za kijeshi, ikiwa ni pamoja na ndege mbili, kulingana na vyombo vya habari vya serikali.
Wizara ya Afya imetuma ambulensi 50 kwenye eneo la tukio, pamoja na maafisa wa idara ya huduma za dharura za kijeshi, ikiwa ni pamoja na ndege mbili, kulingana na vyombo vya habari vya serikali. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwenye mitandao ya kijamii, picha nyingi zilizorushwa mtandaoni zinaonyesha miali mikali ikiteketeza ghorofa nyingi za jengo hilo kubwa la mawe, ambamo huishi askari.

Kati ya "majeruhi 26" waliopelekwa hadi hospitali ya eneo hilo, kulingana na Wizara ya Afya, 24 wanasumbuliwa na "kukosa hewa" na wawili wameungua sana, kulingana na vyombo vya habari vya ndani. Wengine kumi na wawili wametibiwa katika eneo la tukio

Wizara ya Afya imetuma ambulensi 50 kwenye eneo la tukio, pamoja na maafisa wa idara ya huduma za dharura za kijeshi, ikiwa ni pamoja na ndege mbili, kulingana na vyombo vya habari vya serikali.

Moto wa mara kwa mara

Moto, ambao mara nyingi husababishwa na tatizo la umeme,hutokea mara nyingi nchini Misri, nchi ya Kiarabu yenye wakazi milioni 105, yenye miundombinu iliyochakaa na isiyotunzwa vizuri.

Mnamo mwezi Agosti 2022, moto wa bahati mbaya uliua waumini 41 katika kanisa lililokwama kwenye kichochoro katika mtaa wa wafanyakazi wa Cairo, na kusababisha mzozo mkali kuhusu miundombinu na wakati wa majibu wa maafisa wa Zima moto.

Mnamo Machi 2021, takriban watu 20 walifariki kwa tukio la moto katika kiwanda cha nguo katika viunga vya mashariki mwa Cairo, wakati mwaka mmoja mapema, watu kumi na wanne walikufa kwa matukio mawili ya moto katika hospitali mbalimbali nchini kote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.