Pata taarifa kuu

Misri: Takriban watu 41 wafariki katika tukio la moto dhidi ya kanisa mjini Cairo

Katika kanisa la Abu Sifin mjini Cairo, moto ulisababisha vifo vya takriban watu 41 wakati waumini wengi wamekuwa wakihudhuria misa. Hata hivyo moto huo umedhibitiwa.

Moto umezuka wakati wa misa katika kanisa moja katika eneo lenye watu wengi jijini Cairo na kuua watu 41 Jumapili hii, Agosti 14, 2022.
Moto umezuka wakati wa misa katika kanisa moja katika eneo lenye watu wengi jijini Cairo na kuua watu 41 Jumapili hii, Agosti 14, 2022. AP - Mohamed Salah
Matangazo ya kibiashara

Moto ulizuka Jumapili katika kanisa la Abu Sifin katika wilaya ya Imbaba, wakati wa misa. Takriban watu 41 wamefariki dunia na majeruhi wengi kuhamishiwa katika hospitali za karibu. Wizara ya Afya ya Misri imebainisha kuwa imewatambua waathiriwa 55. "Nimezitaka idara zote za serikali ili kuhakikisha kuwa hatua zote zimechukuliwa," Rais Abdel Fattah al-Sissi alijibu mara moja kwenye akaunti yake ya Facebook.

Upande wa mashitaka umetangaza kuwa umefungua uchunguzi na kutuma timu kwenye eneo hilo kubaini sababu za kuzuka kwa moto huo, huku Wizara ya Afya ikieleza kuwa ilituma makumi ya magari ya kubebea wagonjwa.

Abdel Fattah al-Sissi pia ametangaza kwamba "amewasilisha rambirambi zake kwa njia ya simu" kwa kiongozi wa Kanisa la Coptic Tawadros II, akiwa pia mkuu wa jumuiya ya Wakristo nchini Misri tangu mwaka 2012. Tangu wakati huo, Kanisa la Kiorthodoksi la Coptic limekuwa likionekana zaidi katika ulingo wa kisiasa. Chini ya uongozi wa Tawadros II, mfuasi aliyetangazwa wa Abdel Fattah al-Sissi, rais wa kwanza wa Misri amekuwa anahudhuria Misa ya Krismasi ya Coptic kila mwaka, wakati watangulizi wake walikuwa wakikituma wawakilishi.

Cairo, mara kwa mara hukumbwa na mikasa ya moto

Katika jiji kubwa la Cairo, ambako mamilioni ya Wamisri wanaishi katika makazi yasiyo rasmi, mioto ya ajali si jambo la kawaida. Kwa ujumla zaidi, Misri, iliyojaliwa kuwa na miundombinu iliyochakaa na isiyotunzwa vizuri, mara kwa mara hukumbwa na mioto mikali katika majimbo yake mbalimbali.

Mnamo Machi 2021, watu wasiopungua 20 waliaga dunia katika matokeo ya moto katika kiwanda cha nguo katika viunga vya mashariki mwa jijila Cairo. Mnamo 2020, matukio mawili ya moto katika hospitali yalisababisha vifo vya wagonjwa kumi na wanne walio kuwa waliambukizwa Uviko-19 .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.