Pata taarifa kuu

Misri yawasilisha malalamiko ya "ubaguzi wa rangi" wakati wa mechi dhidi ya Senegal

Shirikisho la Soka la Misri, ambalo timu yake ya taifa ilishindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022 baada ya kushindwa na Senegal, imewasilisha malalamiko rasmi dhidi ya Senegal kwa vurugu na "ubaguzi wa rangi", Misri imetangaza.

"Timu ya Misri ilifanyiwa ubaguzi wa rangi baada ya mabango kuonekana kwenye uwanja yakielekezwa kwa wachezaji, hasa Mohamed Salah, nahodha. Yote yameandikwa kwa picha na video zilizoambatanishwa na malalamiko hayo," Shirikisho la Misri limesema katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
"Timu ya Misri ilifanyiwa ubaguzi wa rangi baada ya mabango kuonekana kwenye uwanja yakielekezwa kwa wachezaji, hasa Mohamed Salah, nahodha. Yote yameandikwa kwa picha na video zilizoambatanishwa na malalamiko hayo," Shirikisho la Misri limesema katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii. AP - Stefan Kleinowitz
Matangazo ya kibiashara

Jumanne jioni, Mafarao walipoteza nafasi yao katika Kombe la Dunia la 2022 huko Qatar dhidi ya Simba wa Teranga wa Senegal baada ya mikwaju ya penalti siku ya Jumanne (3-1).

"Timu ya Misri ilifanyiwa ubaguzi wa rangi baada ya mabango kuonekana kwenye uwanja yakielekezwa kwa wachezaji, hasa Mohamed Salah, nahodha. Yote yameandikwa kwa picha na video zilizoambatanishwa na malalamiko hayo," Shirikisho la Misri limesema katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Picha zilizotolewa na shirikisho hilo zinaonyesha kuvunjwa kwa vioo vya basi lililokuwa limebeba Mafarao, mabango ya matusi dhidi ya Mohamed Salah na wananchi wakitoa ishara za matusi kwa wachezaji. Malalamiko rasmi yamewasilishwa kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), linaonyesha Shirikisho la Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.