Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

ICC: Upande wa utetezi waanza kujitetea katika kesi ya kiongozi wa zamani wa Janjawid

Kesi ya Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman, anayejulikana pia kama Ali Kushayb, imeingia katika hatua mpya katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.

Aliyekuwa kiongozi wa Janjaweed Ali Kushayb mbele ya mahakama ya ICC mjini Hague mnamo Mei 24, 2021.
Aliyekuwa kiongozi wa Janjaweed Ali Kushayb mbele ya mahakama ya ICC mjini Hague mnamo Mei 24, 2021. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Hague, Stéphanie Maupas

Akishutumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa mwaka 2003 na 2004 huko Darfur, kiongozi huyo wa zamani wa wanamgambo wa Janjawid, kwa mujibu wa mwendesha mashtaka, amekuwa akisikilizwa tangu mwezi Aprili 2022. Katika hatua ya kwanza ya kesi hiyo, upande wa mashtaka uliita mashahidi 56. hatimaye upande wa utetezi unapewa nafasi ya kujitetea.

Kulingana na wakili wake, mshtakiwa alikuwa mfamasia wa kawaida tu kutoka Garsila huko Darfur, na si mmoja wa viongozi hawa wa janjawid, wanamgambo waliokuwa na uhusiano na utawala wa Omar al-Bashir. Kwa hiyo Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman alikuwa mtu wa kawaida. Hivi ndivyo wakili Cyril Laucci alisema:

"Kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka, alikuwa na jukumu la kuelekeza na kuamuru shughuli zote. Huyu Ali Kushayb si mwakilishi wa serikali wala si afisa wa jeshi. Hajawahi kutuhumiwa na ofisi ya mwendesha mashtaka kwamba alikuwa mwanachama wa Vikosi vya Ulinzi wa raia, Vikosi vya Polisi ya raia au Walinzi wa Mipaka, na bado mtu huyu anaelezewa na ofisi ya mwendesha mashtaka kama mhusika mkuu wa uhalifu huo. "

Wakili huyo pia ameishtmu Sudan. Khartoum ilikataa kutoa viza kwa mawakili na haikutoa hati zilizoombwa, ikiwa ni pamoja na hati ya inayomhusu mshtakiwa. Wakili Cyril Laucci amewakosoa majaji kwa kutoshutumu Sudan mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba ilikataa kutoa ushirikiano wake kama inavyoelezwa katika nakala za Mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.