Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Cameroon: Ishirini wauawa katika shambulio la watu wanaozungumza Kiingereza

Takriban watu ishirini, wakiwemo wanawake na watoto, wameuawa siku ya Jumatatu katika shambulizi dhidi ya kijiji kimoja na watu wanaozungumza Kiingereza wanaotaka kujitenga magharibi mwa Cameroon ambapo waasi hao na jeshi wanapigana kwa miaka saba, maafisa wamesema.

Vikosi vya usalama vya Cameroon vilitumwa baada ya mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga katika kijiji cha Kolofata, Kaskazini Cameroon, Septemba 13, 2015.
Vikosi vya usalama vya Cameroon vilitumwa baada ya mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga katika kijiji cha Kolofata, Kaskazini Cameroon, Septemba 13, 2015. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkasa huo ulitokea usiku katika kijiji cha Egbekaw (mkoa wa Kusini-Magharibi). "Shambulio hilo lilisababisha vifo vya watu ishirini, wanaume, wanawake na watoto, na watu kumi waliojeruhiwa vibaya wako hospitalini," afisa mkuu wa utawala ameliambia shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina.

Tangu mwisho wa 2016, mzozo mbaya unahusisha makundi ya watu wanaopigania uhuru na vikosi vya usalama, kila upande ukituhumiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kwa uhalifu dhidi ya raia, katika mikoa ya Kaskazini-Magharibi na Kusini-Magharibi, inayokaliwa zaidi na watu wachache wanaozungumza Kiingereza ya nchi hii ya Afrika ya Kati yenye watu wengi wanaozungumza Kifaransa.

Waasi "waliwavamia raia wa Egbekaw na idadi ya waliouawa kwa kufikia sasa ni 23 na karibu nyumba kumi na tano zilichomwa moto," afisa wa polisi wa eneo hilo ambaye pia aliomba kutotajwa jina ameliambia shirikala habari la AFP kwa njia ya simu.

Afisa mkuu kutoka Tume ya Haki za Kibinadamu ya Cameroon (CDHC) almmethibitisha shambulio hilo na kutaja ripoti ya muda ya watu waliouawa. "Lakini takwimu hii inaweza kuongezeka," mjumbe wa taasisi hii ya serikali amelihakikishia shirika la habari la  AFP.

Biya, miaka 41 madarakani

Nchini Cameroon, taarifa kuhusu mashambulizi, au vitendo vinavyohusisha vikosi vya usalama, kila mara huwasilishwa rasmi saa kadhaa au hata siku kadhaa baadaye.

Nchi hiyo imetawaliwa kwa mkono wa chuma kwa miaka 41 hadi leo na Rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 90.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio la Egbekaw, lakini habari za mchana kwenye redio na televisheni ya umma zilihusisha "watu wanaotaka kujitenga."

Mzozo huo ulianza mwishoni mwa mwaka 2016 baada ya Paul Biya kukandamiza maandamano ya amani ya watu wanaozungumza Kiingereza katika maeneo hayo mawili, ambao walihisi kutengwa na serikali kuu katika koloni hili la zamani la Ufaransa. Tangu wakati huo, mkuu wa nchi asiyeweza kubadilika ametuma askari kwa wingi katika maeneo hayo.

Mzozo huo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 6,000 na wengine zaidi ya milioni moja kuyahama makazi yao, kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa linalotatua migogoro International Crisi Group (ICG).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.