Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa Urais nchini DRC: Mgombea Delly Sesanga amuunga mkono na Moïse Katumbi

Zikisalia siku kumi na saba kabla ya uchaguzi mkuu nchini DRC, mpinzani na mgombea urais Delly Sesanga amejiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho na kutangaza kumuunga mkono Moïse Katumbi, gavana wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga.

Mwanasiasa wa upinzani na mgombea Delly Sesanga ametangaza kujiondoa kwenye kinyanganyiro cha urais na kumuunga mkono Moïse Katumbi, gavana wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga, kwa uchaguzi wa rais utakaofanyika tarehe 20 Desemba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mwanasiasa wa upinzani na mgombea Delly Sesanga ametangaza kujiondoa kwenye kinyanganyiro cha urais na kumuunga mkono Moïse Katumbi, gavana wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga, kwa uchaguzi wa rais utakaofanyika tarehe 20 Desemba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. © Pascal Mulegwa/RFI
Matangazo ya kibiashara

Hapo awali kulikuwa na wagombea 26, lakini waliosalia ni 22, baada ya wagombea 4 akiwemo Waziri Mkuu wa zamani Matata Poyo kujitokeza nyuma ya Moïse Katumbi.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumapili, Desemba 3 huko Kinshasa, Delly Sesanga amehalalisha chaguo lake kwa kuongeza bahati kwa upande wa upinzani kwa lengo la kumtimua mamlakani Félix Tshisekedi kupitia sanduku ya kura.

Rais anayemaliza muda wake Félix Tshisekedi ni mgombea kwenye kinyang'anyiro cha urais kwa muhula wa pili wa miaka mitano.

"Hii ni kuongeza nafasi ya upinzani ya kuwa na mbadala katika nchi hii. Hii sio chaguo lililofanywa na mtu mmoja. Ni chaguo kuhusiana na mradi wa pamoja ambao tumeunda kwa kuunganisha mapendekezo yetu yote. Pia ni kuhusu uwezekano kwamba kuna, leo, kuunda kambi, muungano ambao unaweza kutoa mtazamo mpya kwa nchi hii na nchi inauhitaji.

"Kutokana na kushindwa dhahiri kwa utawala wa Bw. Tshisekedi anaye maliza muda wake, tunahitaji kwenda zaidi ya kila mmoja kupendekeza kitu tofauti na ndicho tunachofanya. Na mijadala hii lazima iendelee na kila mtu mwingine ambaye anadhani kwamba kuna haja ya kuwa na njia mbadala katika nchi hii.

"Pia tutatoa ulinzi na kujihusisha, kwa makubaliano ya pande zote, na ufuatiliaji wa uchaguzi, kwamba matokeo ya uchaguzi, kituo cha kupigia kura kwa kituo cha kupigia kura, yataheshimiwa. Wananchi lazima wahamasishwe siku moja kuokoa miaka mitano ya maisha yao na hivyo ni dhabihu ya lazima na ya jamhuri,” amesema Delly Sesanga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.