Pata taarifa kuu

DRC: Waangalizi wa kampeni za urais wanashutumu ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa kimsingi

Nchini DRC, wagombea wa uchaguzi wa urais wa Desemba 20 sasa wamekuwa wakiingia mitaani kwa siku kumi na sita kujaribu kuwashawishi wapiga kura milioni 44. Kampeni ambayo ilisababisha machafuko kupita kiasi katika baadhi ya maeneo: katika siku za hivi karibuni, visa kadhaa vya picha za wagombea kuchanwa vimeripotiwa katikamikoa ya Kivu Kaskazini, Katanga na hata Kinshasa.

Maafisa wa polisi wako kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea urais nchini DRC, Martin Fayulu, huko Goma, mashariki mwa DRC, mnamo Novemba 30, 2023.
Maafisa wa polisi wako kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea urais nchini DRC, Martin Fayulu, huko Goma, mashariki mwa DRC, mnamo Novemba 30, 2023. © ALEXIS HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Picha za wagombea zilichanwa: hivi ndivyo Symocel, muungano wa jumbe kadhaa za waangalizi wa uchaguzi, unataja katika taarifa iliyochapishwa Jumatatu hii asubuhi, katika mfumo wa tathmini ya siku za kwanza za kampeni. Symocel pia inaonya dhidi ya haua tatanishi kama vile kupiga marufuku mikutano au usafiri wa ndege kwa wagombea.

Luc Lutala, mratibu wa kitaifa wa Symocel, anatoa wito kwa pande zote kujizuia. "Ni jambo ambalo ni dhahiri kwa watu wanaomkataa mgombea mmoja au mwingine, kwa njia ya kipekee, hutokea kwa mgombea Félix Tshisekedi, au kwa Moïse Katumbi katika matukio machache. Tunatoa wito kwa Wizara ya Mambo ya Ndani kulinda mchakato wa uchaguzi. Tuna imani kwamba wizara hii inajitahidi sana kutimiza wajibu huu. »

“Pia tunatoa wito kwa vyama vya siasa kuongeza uelewa wa wanaharakati wao juu ya kuvumiliana, kuheshimu uhuru wa kimsingi na pia tunatoa wito kwa mamlaka za majimbo zinazovunja na kuminya uhuru wa kimsingi wa wagombea kusimamia sheria badala ya kuchukuwa hatua kwa upendeleo. kwa sababu kwa kuzuia uhuru wa kimsingi, wao pia ni wahusika machafuko yanayosababisha hasira za vyama na wafuasi wa kambi moja au nyingine", amebainisha Luc Lutala, akihojiwa na Gwendal Lavina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.