Pata taarifa kuu

Gaza katikati mwa maadhimisho ya miaka 10 ya kifo cha Mandela nchini Afrika Kusini

Vita vya Gaza vilikuwa kiini cha kumbukumbu ya miaka 10 ya kifo cha Nelson Mandela nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, huku maafisa wakuu wa Hamas wakihudhuria pamoja na familia ya shujaa huyo wa kupinga ubaguzi wa rangi kwenye kumbukumbu hizo mjini Pretoria.

Mjukuu wa Nelson Mandela, Mandla Mandela akiwa amezungukwa na viongozi wakuu wa Hamas.
Mjukuu wa Nelson Mandela, Mandla Mandela akiwa amezungukwa na viongozi wakuu wa Hamas. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Madiba - jina la ukoo wake - alifariki mnamo Desemba 5, 2013 akiwa na umri wa miaka 95. Hakuna sherehe rasmi siku ya Jumanne, wala hotuba nzito kutoka kwa mkuu wa nchi, Cyril Ramaphosa: familia iliweka tu shada la maua alasiri chini ya sanamu ya Mandela mbele ya makao makuu ya serikali katika mji mkuu wa Pretoria.

Maafisa wakuu wa Hamas walikuwepo: Basem Naim, waziri wa zamani wa afya wa Hamas huko Gaza, na Khaled Qaddoumi, mwakilishi wa kundi la wapiganaji wa Hamas kutoka Palestina nchini Iran. Katika siku zilizotangulia, walishiriki katika mkutano kuhusu mzozo wa Israel na Palestina mjini Johannesburg, ulioandaliwa hasa na mjukuu wa Nelson Mandela, Mandla Mandela.

Kuundwa kwa taifa la Palestina kulizingatiwa na babu yake kama "swali kuu la maadili la wakati wetu", amekumbusha kwa idhaa ya kitaifa ya SABC, akisisitiza nia yake ya "kuchukua nafasi".

Afrika Kusini, mtetezi wa dhati wa kadhia ya Palestina, ni mojawapo ya nchi muhimu zaidi zinazokosoa na kulaani mashambulizi makubwa na mabaya ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza, kwa kulipiza kisasi mashambulizi ya umwagaji damu nchini Israel yaliyotekelezwa Oktoba 7 na Hamas. Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Mpakistani Malala Yousafzai, aliyealikwa Johannesburg na Wakfu wa Mandela, kwa upande wake alishutumu "mashambulizi yasio ya haki huko Gaza" wakati wa hotuba yake.

Mwanamke huyo, aliyejulikana mwaka wa 2014 kwa kupigania elimu ya wasichana, pia alichukua fursa hiyo kulaani unyanyasaji wa wanawake nchini Afghanistan, akishutumu utawala wa Taliban kwa kufanya kuwa haiwezekani "kuwa msichana". "Waafrika Kusini walipigania ubaguzi wa rangi uitwe hivyo na kuharamishwa kimataifa," amesisitiza, akitoa wito kwa "ubaguzi wa kijinsia" kuharamishwa sasa.

Mwezi uliopita, wanaharakati mashuhuri wa masuala ya wanawake na watu mashuhuri wa umma walitoa wito kwa Umoja wa Mataifa kurekebisha maandishi ya mkataba unaojadiliwa kuhusu uhalifu dhidi ya binadamu.

"Umaarufu mkubwa"

Ikiwa kutajwa kwa Mandela siku zote kunaonekana kuwa na uwezo wa kuhamasisha maoni ya umma kuhusu sababu zinazopaswa kutetewa, kumbukumbu ya kifo chake ilikuwa na ladha chungu kwa Waafrika Kusini. Kwa wengine, "katika miaka kumi, hakuna mengi ambayo yamebadilika au kuboreshwa" nchini.

Kwa upande mmoja, kumbukumbu ya mfungwa wa zamani kutoka Kisiwa cha Robben ambaye alizika ubaguzi wa rangi na kuleta demokrasia. Kwa upande mwingine, nchi ambayo bado inaongozwa na chama chake, African National Congress (ANC), lakini iliyolemewa na ufisadi, kukatika kwa umeme na kuwa nchi isiyo na usawa zaidi duniani kwa mujibu wa Benki ya Dunia. Na ANC inaweza kushuka chini ya 50% katika uchaguzi mwaka ujao, kulingana na kura za maoni.

Kulingana na balozi wa zamani wa Marekani mjini Pretoria aliyehojiwa na shirika la AFP, Jendayi Frazer, "umaarufu mkubwa" wa Mandela hata hivyo unasalia kuwa "nguvu sana" na kizazi kijacho cha wanasiasa kinapaswa kutazama "mfano wa Mandela na maadili yake ya juu".

Nelson Mandela alifariki dunia akiwa amezungukwa na familia yake baada ya machweo na miezi ya shida, na matatizo kwa Waafrika Kusini na wapenzi wake duniani kote, ambapo wale waliokuwa karibu naye waliridhika kurejelea kwamba mzee huyo alikuwa katika hali ya "mbaya". . Picha yake bado iko sehemu nyingi nchini Afrika Kusini: kwenye noti, kwenye kuta za jiji na uwepo wa sanamu nyingi.

Verne Harris, rais wa muda wa Wakfu wa Mandela na mtunzi wa kumbukumbu wa muda mrefu wa Mandela, anakiri kwamba "hamu ya kina" bado inaonekana miongoni mwa Waafrika Kusini wengi. Lakini "pengine ni wakati wa kumwacha aende, na kutafuta viongozi 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.