Pata taarifa kuu

Guinea: Baada ya mlipuko mbaya, Mamadi Doumbouya atangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa

Idadi ya waliofariki kutokana na moto uliotokea katika bandari ya Conakry baada ya mlipuko wa ghala kuu la mafuta tarehe 18 Desemba imesalia kuwa watu kumi na wanane. Katika kuwaenzi waathiriwa, raiswa mpito wa Guinea Mamadi Doumbouya ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa siku ya Jumatano usiku.

Watu wanatazama eneo la mlipuko wakiwa nyuma ya kizuizi cha usalama baada ya mlipuko wa kituo cha mafuta huko Conakry, Guinea, Desemba 19, 2023.
Watu wanatazama eneo la mlipuko wakiwa nyuma ya kizuizi cha usalama baada ya mlipuko wa kituo cha mafuta huko Conakry, Guinea, Desemba 19, 2023. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia tukio la moto katika ghala kuu la mafuta nchini Conakry, na kusababisha vifo vya watu 18 usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, rais wa mpito, Kanali Mamadi Doumbouya ametangaza Jumatano usiku, siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

"Kutokana na hali hii nzito yenye huzuni, ninatangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu kuanzia Alhamisi, " amesema wakati wa hotuba kwenye televisheni ya serikali.

"Leo, sote tumeguswa sana na msiba huu" , ameongeza Kanali Mamadi Doumbouya, rais wa mpito

"Hakutakuwa na gharama ya ziada"

Na kutokana na wasiwasi wa wananchi wa Guinea kuhusu uhaba wa mafuta, serikali inajaribu kuwahakikishia raia kuhusu uwepo wa mafuta. Kulingana na mamlaka, nchi inaweza kutegemea hisa inayopatikana ya dizeli, kwa sababu matangi matano kwenye bohari kubwa ya Coronthie hayajaathirika. Pia kuna mafuta ya kutosha, kulingana na msemaji wa serikali, ili usafirishaji wa bidhaa na viwanda usiathiriwe na tulio la moto huo.

Bohari ya Coronthie ina uwezo wa kpokea lita milioni 63 za dizeli, milioni 20 za mafuta mazito. Dharura sasa ni usambazaji wa petroli. Nchi hiyo inajadiliana na majirani zake kama vile Côte d'Ivoire kusambaza mafuta hayo katika eneo la Kankan na Sierra Leone kwa mji mkuu Conakry.

Kuhusu wasiwasi wa kupanda kwa bei baada ya hasara iliyosababishwa na moto huo, serikali inawahakikishia wananchi: "Hakutakuwa na gharama ya ziada," imesisitiza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.