Pata taarifa kuu

Guinea: Mlipuko mkubwa wasikika Conakry, na kusababisha majeruhi

Ilikuwa baada ya usiku wa manane siku ya Jumatatu ambapo mlipuko mkubwa ulisikika huko Conakry, na kusababisha moto mkubwa unaowaka juu ya bandari inayojitegemea ya mji mkuu wa Guinea. Kunaripotiwa watu wengi waliojeruhiwa.

Mji mkuu wa Guinea, Conakry, magharibi mwa nchi.
Mji mkuu wa Guinea, Conakry, magharibi mwa nchi. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Conakry, Matthias Raynal

Katika ua wa hospitali ya Donka, mojawapo ya hospitali mbili za chuo kikuu cha Conakry, kumekuwa na msururu wa magari ya kubebea wagonjwa ambayo yamekuwa yakizunguka kwa saa moja. Haiwezekani kutoa tathmini sahihi kwa sasa, lakini mlipuko uliotokea usiku umesababisha watu kadhaa kujeruhiwa.

Gari ndogo lililokuwa na alama ya msalaba mwekundu lilipita uani. Ndani ya gari hilo, alikuwepo mwanamume mmoja aliyekuwa akipiga kelele za maumivu. Pia kuna watu wengi waliojeruhiwa kidogo katika umati wa watu waliojitupa barabarani kuondoka Kaloum.

"Tulikuwa tumelala na ghafla nyumba tulisikia mlipuko mkubwa na kuharibu baadhi ya nyumba. Kila mtu huja na kuondoka, akijaribu kuokoa maisha yake" , amesema Ousmane Barry, mkazi wa mtaa huo.

"Mlipuko huo ulitikisa madirisha ya majengo ya jiji la Conakry ambako kunapatikana wizara na ofisi ya rais. Huko Coronthie, karibu na tukio la mlipuko, kwenye mlango wa kisiwa, wakaazi wameelezea tukio baya. Paa zimedondoshwa na mlipuko huo. Nyumba zilidondoka", ameongeza mkaazi huyo.

Kwenye barabara kuu ya Fidel Castro, saa saba usiku, kumeonekana watu wakitangatanga, kila mtu akijaribu kuokoa maisha yake. Mamia ya watu wamelazimika kutoroka eneo hilo kwa miguu, katikati kabisa ya barabara kuu.

Kwa sasa ni vigumu kuingia au kutoka Kaloum mhi ambao umejaa wanajeshi ambao huruhusu tu magari ya wagonjwa mahututi na viongozi kupita. Raia wa Guinea ambao wana ndugu zao huko Coronthie wanapaswa kuwa na subira.

Wilaya ya Coronthie inajulikana kwa kuhifadhi ghala pekee la mafuta nchini, APT, Kituo cha Mafuta cha Afrika. Wakazi wamekuwa wakiomba kwa miaka mingi kuhamishwakatika eneo lingine mali na jiji hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.