Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Faili ya Cradock Four, mojawapo ya faili za ubaguzi wa rangi kufunguliwa upya

Nchini Afrika Kusini, Wizara ya Sheria ilitangaza Ijumaa, Januari 5, kufunguliwa tena kwa mojawapo ya kesi zinazojulikana zaidi za mauaji ya wanaharakati weusi chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi. "Cradock Four", iliyopewa jina la mji wao kusini mwa nchi, walikuwa wapigania uhuru wanne ambao miili yao ilipatikana ikiwa imechomwa moto na kukatwakatwa mnamo mwaka 1985.

Johannesburg, Mei 8, 2022. Wanawake wanalala kando ya barabara mbele ya Mahakama ya Kikatiba kudai walipwe fidia kama waathiriwa wa utawala wa kibaguzi wa zamani. (Picha ya kielelezo)
Johannesburg, Mei 8, 2022. Wanawake wanalala kando ya barabara mbele ya Mahakama ya Kikatiba kudai walipwe fidia kama waathiriwa wa utawala wa kibaguzi wa zamani. (Picha ya kielelezo) © Claire Bargelès/RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Johannesburg, Claire Bargelès

Licha ya ushahidi uliokusanywa na Tume ya Ukweli na Maridhiano wakati wa kipindi cha mpito mwishoni mwa miaka ya 1990, vyombo vya sheria havikukamilisha uchunguzi.

Tangazo hili lilikaribishwa na familia za wahanga lakini linakuja na mfadhaiko, kwani karibu miaka arobaini imepita tangu uhalifu huu utekelezwe.

“Mshukiwa wa mwisho alifariki dunia hivi karibuni. Hakuna aliyebaki kujibu maswali yetu. Hata hivyo, baada ya mwaka 1994, kulikuwa na matumaini ya kufunguliwa mashtaka. Kamwe hawakulipa kwa matendo yao ya kikatili. Haya yote yanatusikitisha sana,” anasema Nombuyiselo, mjane wa Sicelo Mhlauli, mkuu wa shule wa zamani na mwanaharakati aliyeuawa wakati huo akiwa na umri wa miaka 39 pamoja na wanaume wengine watatu.

Tayari kumekuwa na chunguzi mbili uliofanywa katika miaka ya 80 na 1990 karibu kuhusiana na suala hili lakini bila matokeo. Kisha wajumbe wa vikosi vya usalama walikubali wajibu wao mbele ya Tume ya Ukweli na Maridhiano ... na ombi lao la msamaha lilikataliwa, kwa sababu ya kukiri kutokamilika, lakini tangu wakati huo, hakuna mashtaka yoyote yaliyoanzishwa.

Kulingana na Gina Snyman, wakili wa Wakfu wa Haki za Kibinadamu, hii si kesi ya kutupilia kando.

"Mwishoni mwa Tume ya Ukweli na Maridhiano, faili mia kadhaa zilihamishiwa kwa ofisi ya mashtaka ya Afrika Kusini. Leo, wanashughulikia kesi karibu 135 tu. Sisi wenyewe tunasaidia familia 22, baadhi yao hata hawajaweza kujua walikozikwa wapendwa wao,” Gina Snyman amesema.

Licha ya nia iliyoelezwa na serikali ya Cyril Ramaphosa ya kusonga mbele mambo haya na mabadiliko katika mwaka 2019 kwa mkuu wa ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma wa Afrika Kusini, faili za ubaguzi wa rangi bado ziko mbali na kufungwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.