Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa urais nchini DRC: Ushindi wa Felix Tshisekedi wathibitishwa na mahakama

Mahakama ya Kikatiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumanne imethibitisha kuchaguliwa tena Félix Tshisekedi Tshilombo katika uchaguzi wa urais uliyofanyika Desemba 20, kwa zaidi ya 73% ya kura, baada ya kukataa malalamiko ya mmoja wa wagombea wa uchaguzi huo.

Mahakama ya Kikatiba inayochunguza maombi ya kupinga matokeo ya urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jumatatu hii, Januari 8, 2024.
Mahakama ya Kikatiba inayochunguza maombi ya kupinga matokeo ya urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jumatatu hii, Januari 8, 2024. © Pascal Mulegwa/RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa matokeo ya mwisho yaliyotangazwa katika usikilizaji wa hadhara na Mahakama, rais anayemaliza muda wake, aliye madarakani tangu mwezi wa Januari 2019, amepata sehemu ya kumi ya pointi, kwa asilimia 73.47, ikilinganishwa na takwimu za muda zilizotangazwa Desemba 31 na tume ya uchaguzi (CENI), ambayo ilimpa 73.34% ya kura.

Kwa mujibu wa matokeo ya mwisho yaliyotangazwa katika usikilizaji wa hadhara na Mahakama, rais anayemaliza muda wake, aliye madarakani tangu mwezi wa Januari 2019, amepata sehemu ya kumi ya pointi, kwa asilimia 73.47, ikilinganishwa na takwimu za muda zilizotangazwa Desemba 31 na tume ya uchaguzi (CENI), ambayo ilimpa 73.34% ya kura.
Kwa mujibu wa matokeo ya mwisho yaliyotangazwa katika usikilizaji wa hadhara na Mahakama, rais anayemaliza muda wake, aliye madarakani tangu mwezi wa Januari 2019, amepata sehemu ya kumi ya pointi, kwa asilimia 73.47, ikilinganishwa na takwimu za muda zilizotangazwa Desemba 31 na tume ya uchaguzi (CENI), ambayo ilimpa 73.34% ya kura. © AFP

Ili kufikia matokeo hayo, Mahakama ya Katiba iliondoa katika alama za wagombea 26 wa urais kura zilizorekodiwa katika majimbo mawili ambapo CENI ilifuta uchaguzi mkuu kutokana na udanganyifu mbalimbali. Wakati huo huo, Januari 5, CENI ilifuta kura kwa wagombea 82.

Uchaguzi Mkuu uliyojumuisha - uchaguzi wa urais, wa wabunge wa kitaifa na mikoa pamoja na uchaguzi wa madiwani - ulifanyika mnamo Desemba 20 lakini iliongezwa kwa angalau siku moja kutokana na matatizo mengi ya vifaa.

Takwimu za mwisho zilizoanzishwa na Mahakama ya Kikatiba hazibadilishi orodha ya wagombea 26 ambao walikuwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa urais, uchaguzi wa duru moja, lakini hubadilisha kidogo asilimia ya kura zao walizopata.

Félix Tshisekedi anafuatiwa na gavana wa zamani wa Katanga (kusini-mashariki) Moïse Katumbi, ambaye alipata 18.08% ya kura (bila kubadilika), kisha mpinzani mwingine Martin Fayulu, aliyepata 4.92% (ikilinganishwa na 5 .33% kulingana na takwimu za muda).

Mgombea mwingine, Waziri Mkuu wa zamani Adolphe Muzito, anahesabiwa 1.13% ya kura (ikilinganishwa na 1.12). Wengine wote, akiwemo mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Denis Mukwege, hawazidi 1%.

Siku ya Jumatatu, Mahakama ya Kikatiba ilichunguza ombi la mgombea, ambaye alichukua nafasi ya mwisho katika uchaguzi, aliyeomba kufutwa kwa uchaguzi wa urais, uliogubikwa na "kasoro nyingi", kulingana na mgombea huyo.

Mahakama, ambayo ilitoa uamuzi wake Jumanne kabla ya kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi, ilikataa ombi hili na kutangaza lingine, lililotoka kwa mpiga kura wa kawaida, ambalo halikuweza kukubalika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.