Pata taarifa kuu

DRC: Wakazi wa Kongo bado wanaathiriwa na mafuriko, siku tano baada ya kuanza kupungua

Nchini DRC, wakaazi wa Kongo bado wameathiriwa na mafuriko ingawa mto huo ulianza kupungua Januari 11, kulingana na kituo cha kitaifa cha hali ya hewa. Mikoa kadhaa ya Kongo imekumbwa na hali kama vile nchi hiyo haijapata kutokea tangu mwaka 1961, siku moja baada ya uhuru wake. Maelezo.

Muonekano wa angani unaoonyesha nyumba zikiwa ndani ya maji kutokana na mafuriko katika wilaya ya Mbudi, Kinshasa Januari 9, 2024 kufuatia mvua kubwa na mafuriko ya Mto Kongo.
Muonekano wa angani unaoonyesha nyumba zikiwa ndani ya maji kutokana na mafuriko katika wilaya ya Mbudi, Kinshasa Januari 9, 2024 kufuatia mvua kubwa na mafuriko ya Mto Kongo. AFP - ARSENE MPIANA
Matangazo ya kibiashara

Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakazi wanaoishi karibu na Mto Kongo bado nyumba zao ziko ndani ya maji.

Mikoa kadhaa imekumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mafuriko ya kipekee ya mto huo kama vile DRC haijawahi kushudia tangu 1961, siku moja baada ya uhuru.

Wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa hivi karibuni, mnamo Januari 12, 2024, suala hili lilishughulikiwa kama kipaumbele na serikali inashughulikia mpango wa dharura wa jumla ingawa kupungua kumeanza wiki fupi iliyopita.

Mafuriko yaliyoenea kando ya mto huo ambayo yaliathiri mikoa 14 kati ya 26 ya DRC.

Mto Kongo umezidi mita 6, wakati rekodi ni mita 6 26, na ripoti ya uharibu na vifo ni kubwa kabisa kulingana na mamlaka.

Kwa zaidi ya mwezi mmoja, watu 300 wamekufa kutokana na matokeo ya mafuriko haya na zaidi ya nyumba 43,000 zimeharibiwa. Maelfu ya shule, vituo vya afya, masoko, na pia barabara ziliathiriwa na kiwango hiki cha maji.

Kupungua kulianza Januari 11, kulingana na kituo cha kitaifa cha hali ya hewa. Lakini si pote, kwa sasa. Hali hiyo inashuhudiwa tu magharibi mwa DRC, kutoka Bandundu hadi Kinshasa. Na upungufu huu hutokea mwishoni mwa msimu. Kwa kawaida, katika mko wa Kinshasa, kwa mfano, maji hupungua wakati wa mwezi wa Desemba. Mwanzoni mwa mwezi wa  Januari, kiwango kilikuwa bado kikipanda ulipoingia msimu mfupi wa kiangazi.

Kupungua huku, mamlaka inasema, itachukua muda. Hakuna kurudi kwa hali ya kawaida kabla ya mwezi Februari.

Baadhi ya vitongoji vimekuwa chini ya maji kwa karibu mwezi mmoja sasa. Hali ambayo inazua hofu ya hatari za kiafya, hasa kuibuka kwa magonjwa ya milipuko katika maeneo ya makazi yaliyoathiriwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.