Pata taarifa kuu

Sierra Leone: Rais wa zamani Koroma aruhusiwa kwenda kutibia nje ya nchi

Mahakama ya Sierra Leone siku ya Jumatano ilimruhusu rais wa zamani Ernest Bai Koroma kwenda nje ya nchi kwa matibabu, baada ya kushtakiwa kwa jukumu lake katika madai ya jaribio la mapinduzi mwezi Novemba, wakili wake amesema.

Rais wa zamani wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma.
Rais wa zamani wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

 

"Mahakama Kuu ya Sierra Leone Jumatano ilitoa dhamana kwa Rais wa zamani Ernest Bai Koroma ili aweze kupata matibabu nje ya nchi," Joseph Fitzgerald Kamara aliambia wanahabari, bila kutaja tarehe ya kuondoka kwake.

Bw. Koroma, 70, ambaye aliongoza nchi kutoka mwaka 2007 hadi 2018, atakwenda nchini Nigeria kupata matibabu, Mahakama Kuu imeandika katika ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa X. Alishtakiwa mapema mwezi wa Januari kwa makosa manne, ikiwa ni pamoja na uhaini na kuficha uhaini.

Rais huyo wa zamani alitakiwa kuripoti mahakamni siku ya Jumatano lakini kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 6, wakili wake amesema. Kulingana wakali wake, Bw. Koroma, anayezuiliwa nyumbani tangu Desemba 9, pia ana idhini ya kuondoka nyumbani kwake kutafuta matibabu.

Mapema Novemba 26, watu waliojihami kwa bunduki za kivita walishambulia ghala la kijeshi, kambi nyingine mbili, magereza mawili na vituo viwili vya polisi, wakikabiliana na vikosi vya usalama. Mapigano hayo yalisababisha vifo vya watu 21, wanajeshi 14, askari polisi, askari magereza, maafisa wa usalama, mwanamke mmoja na washambuliaji watatu, kwa mujibu wa Waziri wa Habari.

Takriban watu 80 walikamatwa kuhusiana na matukio haya, hasa askari, 27 kati yao walifunguliwa mashitaka ya "uasi." Bwana Koroma alihojiwa mara kadhaa na polisi.

Ujumbe wa ngazi ya juu kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), ukiongozwa na marais wa Senegal na Ghana, ulikutana na Bw. Koroma na Rais wa sasa Julius Maada Bio mwishoni mwa mwezi wa Desemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.