Pata taarifa kuu

DRC: Nyumba na mashamba kadhaa yasombwa na maji ya mvua Bukama

Nyumba na mashamba kadhaa yamejaa maji kwa siku kadhaa na mengine yamesombwa na maji katika eneo la Bukama (Haut-Lomami) kufuatia mafuriko yanayotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika eneo hilo.

Kinshasa, DRC, Barabara kuu ya Juni 30 yakumbwa na mafuriko, Oktoba 25, 2019.
Kinshasa, DRC, Barabara kuu ya Juni 30 yakumbwa na mafuriko, Oktoba 25, 2019. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

 

Kulingana na Radio Okapi ikimnukuu mkazi wa Bukama, mamia ya nyumba na mashamba yamesombwa na maji.

"Katika wilaya ya Kisanga wa Bioni, kuna zaidi ya nyumba 400 ambazo zimejaa maji, katika wilaya ya Lualaba kuna nyumba zaidi ya 200 ambazo pia zimejaa maji," inabainisha Radio Okapi ikimnukuu Kevin Kyange, mkazi wa Bukama.

Mbali na nyumba, vituo viwili vya afya pia vimeathiriwa, radio Okapi inaongeza.

“Bado kuna vituo viwili vya afya ambavyo vimejaa maji. Kuna kituo cha afya katika wilaya ya Lualaba na kituo katika wilaya ya Kisanga wa Bioni,” anasimulia mzaliwa huyu wa Bukama.

Anasema kuwa familia zilizoathiriwa zimeacha nyumba zao na wengine wanalala nje usiku, bila msaada kupata wowote:

“Hawana mahali pa kukaa. Wapo kituoni wanalala nje na watoto. Katika maeneo ambayo ni chafu na pia yenye ukosefu wa usalama.”

Mashirika ya kiraia yanahofia magonjwa kwa sababu watu hawa walioathirika wanakabiliwa na hali mbaya ya hewa na eneo hilo linakabiliwa na mlipuko wa Kipindupindu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.