Pata taarifa kuu

Mapigano kati ya al-Shabab na jeshi la serikali yaripotiwa Somalia

Nairobi – Mapigano mazito yameripotiwa katikati mwa nchi ya Somalia baada ya wapiganaji wa al-Shabab kushambulia kambi za jeshi katika eneo la Mudug.

Mapigano mazito yameripotiwa katikati mwa nchi ya Somalia baada ya wapiganaji wa al-Shabab kushambulia kambi za jeshi katika eneo la Mudug
Mapigano mazito yameripotiwa katikati mwa nchi ya Somalia baada ya wapiganaji wa al-Shabab kushambulia kambi za jeshi katika eneo la Mudug AP - Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Mashuhuda jijini Mogadishu wameiambia BBC kuwa wamesikia milio mizito ya risasi na milipuko mapema leo Jumatano.

Shambulio hilo limeripotiwa kutokea baada ya mlipuaji wa kujitoa mhanga kuvilenga vitengo maalum vya jeshi la serikali.

Waziri wa usalama katika eneo la Galmudug Mohamed Abdi Aden, ameiambia BBC kwamba wanajeshi wa serikali walikuwa wanakabiliana na wapiganaji hao katika kijiji cha Aad, ambapo kambi za kijeshi zinapatikana.

Nalo shirika la habari la kitaifa nchini humo (Sonna) limeripoti kwamba jeshi kwa ushirkiano na wakaazi limetibua shambulio, hali ambayo imesababisha hasara kubwa kwa adui.

Al-Shabab kwa upande wao wamedai kuteka kambi tano za jeshi na kuwaua mamia ya wanajeshi.

Tangu mwezi Agosti mwaka wa 2022, serikali ya Somalia imekuwa ikiteleza mashambulio katika ngome za kundi hilo linalohusishwa na al-Qaeda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.