Pata taarifa kuu

ICC yatoa wito kwa baraza la usalama la UN kuchukua hatua kuzuia mauji Sudan

Nairobi – Mwendesha mashataka mkuu wa mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita, ICC, amelitaka baraza la usalama la umoja wa Mataifa, kuchukua hatua za haraka, kukomesha mauaji ya kiholela yanayoshuhudiwa Sudan na hasa kwenye jimbo la Darfur.

 Karim Khan - Mwendesha mashataka wa ICC
Karim Khan - Mwendesha mashataka wa ICC REUTERS - PIROSCHKA VAN DE WOUW
Matangazo ya kibiashara

Karim Khan ameeleza kuwa ofisi yake inakusanya ushahidi muhimu unaonyesha kuwa wanajeshi wa serikali ya Sudan na wapiganaji wa RSF wametekeleza visa vya mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita na ukiukaji mwengine wa haki za binadamu katika jimbo hilo la Darfur.

Ofisi ya Khan ilianza kufanya uchunguzi mwezi Julai mwaka uliopita, muda mfupi baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa RSF.

Wapiganaji wa RSF nchini Sudan wamekuwa wakipigana na jeshi la serikali
Wapiganaji wa RSF nchini Sudan wamekuwa wakipigana na jeshi la serikali AFP - -

Mji wa Darfur ni mojawapo na maeneo ambayo yameathiriwa pakubwa na mapiganao yanayoendelea nchini Sudan.

Zaidi ya watu nusu milioni wametoroka nchini Sudan kuelekea katika taifa jirani la Chad kwa hofu ya kushambuliwa katika vita vinavyoendelea.

Maelfu ya raia wa Sudan wametorokea katika nchi jirani ya Chad wakihofia mapigano yanayoendelea
Maelfu ya raia wa Sudan wametorokea katika nchi jirani ya Chad wakihofia mapigano yanayoendelea © Zohra Bensemra / Reuters

Aidha Khan ameonya kuwa hali katika mji wa Darfur inaendelea kuwa mbaya, akitoa wito kwa mamlaka nchini Sudan kushirikiana na mahakama ya ICC katika uchunguzi huo.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakiwatuhumu wapiganaji wa RSF na washirika wao kwa kuhusika na mauaji ya kikabila dhidi ya jamii ya Masalit, Magahribi mwa Darfur.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.