Pata taarifa kuu
SIASA-USALAMA

Raia wa Guinea kujiua katika kituo cha kizuizini: Sintofahamu yazuka Italia

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Italia imefungua uchunguzi baada ya mtafuta hifadhi kutoka  Guinea kujiua katika kituo cha kizuizini. raia huyo alikuwa akiishi nchini Italia kwa miezi kadhaa katika kituo hiki kinachokosolewa na mashirika yasiyo ya kiserikali, kulingana na shirika la habari la AFP likinukuu chanzo cha mahakama.

Kiongozi wa mrengo mkali wa kulia Giorgia Meloni akiwa mkuu wa serikali ya Italia aliwaahidi wapiga kura wake kuzuia boti za wahamiaji kuvuka bahari ya Mediterania.
Kiongozi wa mrengo mkali wa kulia Giorgia Meloni akiwa mkuu wa serikali ya Italia aliwaahidi wapiga kura wake kuzuia boti za wahamiaji kuvuka bahari ya Mediterania. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Ousmane Sylla, 22, alijinyonga siku ya Jumapili katika kituo cha makazi cha wageni (CPR) karibu na Roma. Katika ujumbe kwa lugha ya Kifaransa kwenye ukuta wa kituo hicho, aliandika: "Ikiwa nitakufa, ningependa mwili wangu urudishwe Afrika." Mwendesha mashtaka alifungua uchunguzi kwa "uchochezi wa kujiua" na akaamuru uchunguzi wa maiti, kulingana na chanzo hiki.

Kifo cha kusikitisha cha mhamiaji huyo mchanga ambaye ombi lake lilikataliwa kilichochea hasira ya watu wengine waliokuwa kizuizini ambao walichoma magodoro na kuwarushia polisi vitu. Makabiliano hayo yaliendelea siku nzima ambapo watu 14 kutoka Morocco, Cuba, Chile, Senegal, Tunisia, Nigeria na Gambia walikamatwa, carabinieri wamesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Takriban watu mia moja waishi katika kituo cha kizuizini kinachozungumziwa, "kuzimu" ambapo wahamiaji wananyimwa uhuru wao katika "hali zisizo za kibinadamu", kulingana na katibu mkuu wa chama cha mrengo wa kushoto cha +Europa, Riccardo Magi. Pamoja na Chama cha Kidemokrasia na Muungano wa Kijani na Kushoto, waliwasilisha mpango katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu wakitaka vituo hivi vifungwe. "Mfumo wa kizuizini nchini Italia unaporomoka, iwe katika vituo vya magereza au CPRs," alisema Bw. Magi.

Kiongozi wa mrengo wa kulia Giorgia Meloni, mkuu wa serikali ya kihafidhina tangu Oktoba 2022, aliwaahidi wapiga kura wake kuzuia boti za wahamiaji zinazovuka bahari ya Mediterania kufika Ulaya. Lakini mwaka jana, karibu watu 158,000 walitua kwenye mwambao wa Italia, ongezeko kubwa ikilinganishwa na mwaka 2022 (105,131).

Roma hivi majuzi ilitia saini makubaliano yenye utata na Albania ikitoa nafasi ya kuunda vituo vya kupokea wahamiaji katika ardhi ya Albania, vinavyosimamiwa na kufadhiliwa na Italia. Makubaliano yaliyotiwa muhuri "kwa kukosekana kwa dhamana ya kutosha katika suala la haki za binadamu", alishutumu mnamo Desemba Kamishna wa Haki za Binadamu wa Baraza la Ulaya, Dunja Mijatović, akipendekeza kwamba Italia "uboreshaji wa fursa ya hifadhi ya kitaifa na mifumo ya mapokezi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.