Pata taarifa kuu

Guinea: Utawala wa kijeshi wafunga akaunti za benki za maafisa wa serikali iliyovunjwa

Utawala wa kijeshi nchini Guinea umeagiza kufunwa kwa akaunti za benki na kutwaliwa kwa pasipoti za wajumbe wa serikali baada ya kuivunja serikali kwa sababu ambazo bado hazijajulikana.

Mamadi Doumbouya, rais wa mpito wa Guinea.
Mamadi Doumbouya, rais wa mpito wa Guinea. © RFI
Matangazo ya kibiashara

 

Siku ya Jumatatu wanajeshi ambao walichukua madaraka kwa nguvu mnamo mwezi Septemba 2021 walitangaza kuvunjwa kwa serikali ambayo walikuwa wameiweka mnamo mwezi Julai 2022.

Wameamua kufungia akaunti za wajumbe wa serikali, kuchukua hati zao zote za kusafiri, pamoja na magari yote ya kazi, na kuwany'anganya walinzi wao na wasaidizi wao, inabaini taarifa iliyosomwa siku ya Jumatatu jioni kwenye runinga ya serikali na Jenerali Ibrahima Sory Bangoura, mkuu wa majeshi, mbele ya askari wengine ishirini.

Hakuna maelezo ambayo yametolewa hadharani kwa hatua hizi, wala kwa kuvunjwa kwa serikali. Watawala wa Guinea, kama wale ambao wamejidhihirisha katika nchi kadhaa za Afrika Magharibi tangu 2020, wamefanya vita dhidi ya ufisadi kuwa moja ya maneno yake.

Mvutano uliripotiwa hivi karibuni kati ya wajumbe wa serikali. Mji mkuu wa Conakry ulikumbwa na tukio la maandamano mwanzoni mwa mwezi wa Februari, kipindi cha maandamano ambacho kilikuwa nadra sana chini ya utawala wa kijeshi, ambao ulipiga marufuku maandamano yoyote. Ulikandamiza upinzani, ambao kwa kiasi kikubwa ulidhoofiswa na kutokuwa na uwezo. Nchi imekuwa ikikabiliwa na vikwazo vikali vya ufikiaji wa mtandao kwa wiki kadhaa. Utawala wa kijeshi umevishambulia vyombo kadhaa vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.