Pata taarifa kuu

Somalia yawahukumu kifo raia sita wa Morocco wanaohusishwa na IS

Mahakama ya kijeshi kaskazini mwa Somalia imewahukumu kifo raia sita wa Morocco kwa kujihusisha na kundi la Islamic State.

Nchi hiyo dhaifu katika Pembe ya Afrika imekuwa ikikabiliwa na uasi wa miaka 17 unaoongozwa na kundi la Al-Shabab lenye mafungamano na Al-Qaeda, na wanamgambo wa kundi la Islamic State pia wanaendesha harakati zao nchini humo.
Nchi hiyo dhaifu katika Pembe ya Afrika imekuwa ikikabiliwa na uasi wa miaka 17 unaoongozwa na kundi la Al-Shabab lenye mafungamano na Al-Qaeda, na wanamgambo wa kundi la Islamic State pia wanaendesha harakati zao nchini humo. © MOHAMED ABDIWAHAB / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Nchi hiyo dhaifu katika Pembe ya Afrika imekuwa ikikabiliwa na uasi wa miaka 17 unaoongozwa na kundi la Al-Shabab lenye mafungamano na Al-Qaeda, na wanamgambo wa kundi la Islamic State pia wanaendesha harakati zao nchini humo. Siku ya Alhamisi, Ali Dahir, makamu wa rais wa mahakama ya kijeshi ya Bossaso, katika jimbo la Puntland, aliwahukumu kifo raia sita wa Morocco kwa kujaribu "kuharibu maisha yao, yale ya jamii ya Kiislamu, ya watu wa Somalia na kusababisha machafuko nchini humo.

Mahakama hiyo pia imemhukumu raia wa Ethiopia na raia wa Somalia kifungo cha miaka 10 jela kuhusiana na kesi hiyo. Mwendesha mashtaka Mohamed Hussein amewaambia waandishi wa habari kuwa raia hao sita wa Morocco wamekamatwa huko Puntland na kwamba uchunguzi umekuwa ukiendelea kwa takriban mwezi mmoja.

Al-Shabab walifukuzwa kutoka Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, mwaka 2011 na kikosi cha Umoja wa Afrika, lakini kundi hilo bado linadhibiti maeneo makubwa ya mashambani na linaendelea kufanya mashambulizi mabaya dhidi ya malengo ya kiraia, kisiasa na kijeshi. Mwaka jana, uvamizi wa kijeshi wa Marekani kaskazini mwa Somalia, ulioamriwa na Rais Joe Biden, uliua kiongozi mkuu wa IS katika eneo hilo. Bilal al-Sudani alikuwa na jukumu la kufadhili operesheni za IS, sio tu barani Afrika bali pia nchini Afghanistan.

Vikosi vya Marekani siku za nyuma vilishirikiana na wanajeshi wa Umoja wa Afrika na wanajeshi wa Somalia katika operesheni za kukabiliana na ugaidi na wamefanya uvamizi na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye kambi za mafunzo za Al-Shabab kote nchini Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.